Numidia ni eneo la kihistoria katika Afrika ya Kaskazini. Leo hii ni sehemu ya nchi za Tunisia na Aljeria.

Numidia ya kihistoria

Ilijulikana katika karne za KK kama eneo la Wanumidia waliokuwa tawi la Waberberi.

Baada ya kufika kwa Wafinisia waliounda makoloni kama Karthago na kutawala pwani, Wanumidia walisukumwa kwenda milima ya Atlasi na mitelemko yake.

Ufalme wa Numidia hariri

Mnamo mwaka 200 wakati wa vita ya pili ya Waroma dhidi Karthago Massinissa aliunda ufalme wa Numidia iliyotawala nchi kati ya Karthago na ufalme wa Mauritania upande wa magharibi.

Mtoto wake Yugurtha aliendesha vita kali dhidi ya Roma lakini alishindwa. Wakati wa karne ya kwanza KK Numidia ilikuwa nchi lindwa chini ya Roma.

Mfalme wa mwisho wa Numidia alishiriki katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Waroma upande wa Pompeio lakini alishindwa na Caesar.

Jimbo la Kiroma hariri

Tangu mwaka 46 BK nchi ikawa jimbo la Dola la Roma kwa jina la "Numidia Cirtensis". Numidia ilistawi kiuchumi na kiutawala. Miji mingi ilianzishwa na kuendelea vizuri.

Baada ya mwaka 400 kuna taarifa ya maaskofu 123 kutoka Numidia waliokutana kwenye sinodi za Karthago. Wakati ule askofu alipatikana tu katika mji wenye umuhimu fulani na idadi hii ni dalili ya maendeleo inayoonekana leo hii kutokana na maghofu mengi.

Wavandali na Waarabu hariri

Tangu kuingia kwa Wavandali hali ya uchumi ilizorota. Mashamba hayakulimwa tena na jangwa lilipanuka.

Kuja kwa Waarabu hakusaidia kushuka kwa hali ya maisha kulingana na kale za Waroma.