Damietta
Damietta, Damiata, au Domyat (Kiarabu: دمياط) ni kituo cha safari za Majini, au bandari na pia ni mji mkuu wa uongozi wa Domyat, wa nchini Misri. Ipo katika sehemu ya mwingiliano katika ya bahari ya Mediterania na Mto Nile na pia ipo upande wa kaskazini mwa Cairo
Jiji la Damietta | |
Mahali pa mji wa Damietta katika Misri |
|
Majiranukta: 31°25′0″N 31°49′0″E / 31.41667°N 31.81667°E | |
Nchi | Misri |
---|---|
Mkoa | Damietta |
Tovuti: www.damietta-port.gov.eg |
Historia
haririKatika Misri ya kale, mji huu ulikuwa unajulikana kama Tamiat, lakini uliendelea kupoteza umuhimu kufuatia kuja kwa ustaarabu wa Helleic, muda mfupi baada ya kujengwa kwa Alexandria.
Wakazi wa Abbasids hutumia vituo vya Alexandria, Damietta, Aden na Siraf kama njia katika kuingia katika nchi za India na China.[1]
Damietta na ilikuwa umuhimu sana katika karne ya 12 na 13 wakati wa vita vya kidini hususani vya kikristo. Mnamo mwaka 1169, wakitokea katika ufalme wa Jerusalem kwa msaada wa Ufalme wa Byzantine walivamia na kushambulia mji wa Damietta lakini walishindwa na kupigwa na Saladin.
Katika maandalizi ya vita vya tano vya kidini mwaka 1217, iliamuliwa kuwa, mji wa Damietta ndio ungekuwa shabaha ya mashambulizi kwani kwa kuweza kuwa na mamlaka juu ya mji wa Damietta kungesabisha mamlaka pia juu ya mto Nile, na kwa kuanzia hapo wapiganaji hawa wa vita vya kidini wangeweza kuwa na mamlaka juu ya Nchi ya Misri. Na kwa kutokea nchini Misri wangeweza kushambulia nchini ya Palestine na kuuteka mji wa Jerusalem
Wakati mji wa Damietta ulipozungukwa na kukaliwa na Frisia katika vita vya kidini vya mwaka 1219, Francis wa Asisi alifika katika mji huo, na kufanya mazungumzo ya amani na kiongozi wa kiislamu wa eneo hilo. Mwezi Oktoba mwaka 1218. Viongozi mbalimbali walifika katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na wanaharakati wa kiingereza kama vile Ranulf of Chester, Saer of Winchester na William Aubigny Odonel Aubigny, Robert Fitz Walter, John Lacy wa Chester, William Harcourt na Oliver aliyekuwa mtoto wa nje ya ndoa wa King John.[2] Mwaka 1221, wapiganaji hawa wa vita vya kidini walijaribu kuingia katika mjiwa Cairo lakini walishindwa kutoka na kupata upinzani mkali kutoka kwa waislamu.
Damietta pia ilikuwa ni shabaha la wapiganaji wa dini ya kisabato, Seventh Crusade, wakiongozwa na Louis IX of France. Majeshi yake yalifaika katika mji huo mwaka 1249 na kuweza kuuteka mji huo katika kipindi kifupi, lakini alikataa kuukabidhi mji huo kwa wahitaji wake wa kwanza yaani mfalme wa Jerusalem. Ambaye ndiye aliyeahidiwa katika vita vya tano. Lakini baada ya muda mfupi, Louis aliangushwa na kunyang'anywa mamlaka juu ya mji huo. Kutokana na umuhimu wa mji huo, kwa wapiganaji wa kidini, Sultani Mamluk aliubomoa mji huu na kuujenga kilometa chache kutoka ilipo bandari.
Majengo
hariri- Amr Ibn Al-a'as Msikiti wa (Al-Fateh) ndio msikiti wa pili kujengwa na waarabu baada tu ya kuingia katika nchi ya Misri. Ulishabadilishwa na kuwa kanisa mara mbii kutokana na wapiganaji wa kikristo. Louis IX of France son Jean Tristan aliyekuwa mtoto wa Jean Tristan alibatizwa na makamu wa papa katika msikiti huu.
- Al-Matbuly Mosque dating to Mamluk era.
- Msikiti wa Al-Maainy kuanzia kipindi cha uongozi wa Al-Naser Mohammed Ibn Qalawon.
- Msikiti wa Al-Bahr kuanzia kipindi cha uongozi wa Ottmo.
- Msikiti wa Al—Hadidy uliopo katika eneo la Faraskour miaka 200 iliyopita.
- Tabiet Ahmed Urabi, ruins of Damietta Fort at Ezbet El-Borg.
- Msikiti wa Al-Radwaniya tangu enzi za Mamluk.
- Daraja la zamani la " Elkobri Elqadeem" kuanzia miaka ya mwanzoni ya 1900.
- Mji wa zamani wa Souk Al-Hesba,tangu uongozi wa Abbasi.
Damietta hii leo
haririLeo hii, kuna mfereji unaounganisha mji huu na Mto Nile ambapo ndio inaufanya mji huu kwa wa muhimu kwa mara nyingine tena. Mji huu kwa sasa una idadi ya watu wapatao 1,093,580 (2006). Pia kuna mtambo wa gesi ya SEGAS LNG (Liquefied Natural Gas) ambao hapo baadaye utakuwa na uwezo wa kuwa na ujazo kiasi cha tani 9.6 kwa mwaka.
Shughuli za Kiuchumi
hariri- White Dammiat Cheese (Domiati) na bidhaa nyingine nyingi ambzo zimeenea kote Misri, Greece, Kupro, Sudan na Uturuki.
- Ufundi seremala na utengenezaji wa samanis
- Pattisiare and Egyptian desserts.
- Ushonaji
- Usafirishaji mizigo mikubwa
- Uvuvi
Marejeo
hariri- ↑ Donkin, Robin A. (2003). Between East and West: The Moluccas and the Traffic in Spices Up to the Arrival of Europeans. Diane Publishing Company. ISBN 0871692481.
- ↑ Remfry, P.M., (1997). Buckenham Castles, 'The Aubignys and the Fifth Crusade, 1218 to 1221'. ISBN 1-899376-05-4.
Viungo vya nje
hariri- (Kiarabu) (Kiingereza) Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 13 Februari 2010 kwenye Wayback Machine.
- Falling Rain Genomics, Inc. "Geographical information on Dumyat, Egypt". Iliwekwa mnamo 2008-03-22.