Door of Hope Tanzania

Door of Hope to Women and Youth Tanzania (kwa Kiswahili Milango ya matumaini kwa wanawake na vijana Tanzania) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyopo katika kata ya Shangani, manispaa ya Mtwara, Tanzania. Ni shirika linaloshugulika kuwainua kina mama na vijana kiakili, kisaikolojia na kimwili ili waweze kufanikiwa na kuwa na maendeleo endelevu [1].

Malengo hariri

Malengo ya asasi hiyo ni kusaidia na kuwawezesha wanawake na vijana katika maendeleo ya kiuchumi na kukuza ushiriki wa vijana na kina mama katika maendeleo ya umma.

Hapo mwanzo, asasi hiyo ilikuwa ikijulikana kama Tanzania Youth and Women Foundation.

Asasi hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2016.

Tanbihi hariri