Umandejua
Umandejua | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Umandejua (Drosera tokaiensis)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Mimea ya Umandejua inaainishwa kwenye jenasi Drosera ambayo ni mojawapo ya jenasi kubwa zaidi ya mimea ambayo hula nyama. Jenasi ya Drosera ina angalau spishi 194[1]. Mimea hii ya familia ya Droseraceae huwavutia, kuwashika na kuwaua wadudu kwa kutumia viungo vyenye kuzalisha maji yenye gundi. Wadudu hawa hupendwa na umandejua kwa sababu mmea wenyewe unamea katika ardhi isiyokuwa na rotuba ya kutosha. Spishi mbalimbali, ambazo huwa na maumbo tofauti, hupatikana katika mabara yote isipokuwa Bara la Antaktiki.
Sifa za mmea
haririUmandejua ni mimea inayodumu kwa miaka nyingi (lakini baadhi ya spishi hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu). Ina maua madogomadogo yaliyosimama ambayo ni karibu sm 1 na m 1 kwa urefu ikitegemea ni spishi ipi. Spishi zinazopanda huwa na shina zinazoweza kuwa ndefu sana hata kufikia mita 3, kama vile D. erythrogyne[2].
Imebainika kuwa mmea wa umandejua unaweza kuishi kwa kipindi cha hata miaka 50.[3] Jinasi hii imezoea zaidi kupata chakula kupitia kula wadudu kiasi kwamba enzaimu ya aina ya naitreti riadaktesi[4]) ambayo kawaida hutumiwa na mimea kupandishia nitrati haipo.
Picha
hariri-
Maua ya umande jua wa spishi ya D. kenneallyi
-
Kusonga kwa matawi katika spishi moja ya umande jua
-
Matawi ya umande jua wa kawaida (Drosera rotundifolia)
-
Mdudu aliyekamatwa katika umande jua
Maandiko ya chini
hariri- ↑ McPherson, S.R. (2010). Carnivorous Plants and their Habitats. Poole: Redfern Natural History Productions Ltd. 2 volumes.
- ↑ Mann, Phill (2001). The world's largest Drosera Archived 29 Septemba 2011 at the Wayback Machine.; Carnivorous Plant Newsletter, Vol 30, #3: pg 79.
- ↑ Barthlott et al., Karnivoren, p. 102
- ↑ Karlsson PS, Pate JS (1992). "Contrasting effects of supplementary feeding of insects or mineral nutrients on the growth and nitrogen and phosphorus economy of pygmy species of Drosera". Oecologia. 92: 8–13. doi:10.1007/BF00317256.
Marejeo
haririVitu vingi katika makala haya vinatoka katika tafsiri ya Kijerumani ya makala haya ya wikipedia article (retrieved 30 Aprili 2006).
- Barthlott, Wilhelm; Porembski, Stefan; Seine, Rüdiger; Theisen, Inge: Karnivoren. Stuttgart, 2004, ISBN 3-8001-4144-2
- Correa A., Mireya D.; Silva, Tania Regina Dos Santos: Drosera (Droseraceae), in: Flora Neotropica, Monograph 96, New York, 2005
- Darwin, Charles: Insectivorous Plants, 1875
- Lowrie, Allen: Carnivorous Plants of Australia, Vol. 1-3, English, Nedlands, Western Australia, 1987 - 1998
- Lowrie, Allen: A taxonomic revision of Drosera section Stolonifera (Droseraceae) from south-west Western Australia, 2005, Nuytsia 15(3):355-393. (Online: http://science.calm.wa.gov.au/nuytsia/15/3/355-394.pdf Archived 19 Agosti 2006 at the Wayback Machine.)
- Olberg, Günter: Sonnentau, Natur und Volk, Bd. 78, Heft 1/3, pp. 32–37, Frankfurt, 1948
- Rivadavia, Fernando; Kondo, Katsuhiko; Kato, Masahiro und Hasebe, Mitsuyasu: Phylogeny of the sundews, Drosera (Droseraceae), based on chloroplast rbcL and nuclear 18S ribosomal DNA Sequences, American Journal of Botany. 2003;90:123-130. (Online: http://www.amjbot.org/cgi/content/full/90/1/123)
- Seine, Rüdiger; Barthlott, Wilhelm: Some proposals on the infrageneric classification of Drosera L., Taxon 43, 583 - 589, 1994
- Schlauer, Jan: A dichotomous key to the genus Drosera L. (Droseraceae), Carnivorous Plant Newsletter, Vol. 25 (1996)
Viungo vya nje
hariri- A key to Drosera species, with distribution maps and growing difficulty scale Archived 18 Februari 2008 at the Wayback Machine.
- A virtually exhaustive listing of Drosera pictures on the web Archived 1 Septemba 2006 at the Wayback Machine.
- International Carnivorous Plant Society
- Carnivorous Plant FAQ
- Listing of scientific Drosera articles online (terraforums.com) Archived 24 Novemba 2007 at the Wayback Machine.
- The Sundew Grow Guides Archived 19 Februari 2010 at the Wayback Machine.
- Sundew images from smugmug
- Botanical Society of America, Drosera - the Sundews Archived 13 Juni 2010 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Umandejua kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |