Duaradufu
Duaradufu ni neno la kutaja maumbo ya jiometria yanayofanana na duara. Kwa lugha ya kawaida ni umbo linalofanana na yai la ndege. Katika mazingira yetu obiti za sayari yaani njia ambako sayari zinazunguka jua huwa na umbo la duaradufu.
Kwa maana duaradufu (ing.: oval) ya jiometria ni mchirizo uliofungwa kwenye bapa moja. Kuna angalau mhimili 1 inayogawa umbo kwa nusu 2 sawa. Hapo duara ni mfano mmoja wa maumbo yanayoweza kuitwa duaradufu
Kwa maana ya pekee duaradufu ([[en:ellipse) ni umbo linalopatikana wakati bapa inakata gimba la pia kimsharazi na pande mkabala za pia kwa namna ya kuleta mchirizo uliofungwa.
Kwa mtazamo huu duara ni hali ya pekee ya duaradufu inayopatikana kama bapa inakata pia kwa nyuzi sulubi (90°) kwa mhimili wa pia.
Duaradufu huwa na fokasi mbili isipokuwa hali ya pekee ya duara fokasi zko mahali pamoja ambapo ni kitovu chake.
Kihisabati duaradufu ni jumla ya nukta zota za bapa ambazo maumbali ya kila nukta kutoka kwenye nukta mbili fungwa F1 na F2 ni sawa.
Viungo vya Nje
- Ellipse & Hyperbola Construction Archived 11 Februari 2008 at the Wayback Machine. - An interactive sketch showing how to trace the curves of the ellipse and hyperbola. (Requires Java.)
- Ellipse Construction - Another interactive sketch, this time showing a different method of tracing the ellipse. (Requires Java.)
- Ellipse on MathWorld - More on Ellipse
- The Shape and History of The Ellipse in Washington, D.C. by Clark Kimberling
- Collection of animated ellipse demonstrations. Ellipse, axes, semi-axes, area, perimeter, tangent, foci.
- Woodworking videos showing how to work with ellipses in wood.
References