Dubai (kwa Kiarabu: دبيّ) ni mji mkuu wa ufalme wenye jina hilo katika katika Shirikisho la Falme za Kiarabu kwenye rasi ya Uarabuni.

Mji wa Dubai

Uko kwenye mwambao wa Ghuba ya Uajemi kati ya Sharjah na Abu Dhabi.

Jiji la Dubai lilikuwa mji mdogo wenye wakazi 20,000 tu hadi vita kuu ya pili ya dunia. Leo hii kuna wakazi zaidi ya 1,200,000. Nyumba zote za Dubai ni mpya.

Kukua kwa Dubai kulitokana na mapato ya mafuta ya petroli. Lakini akiba za mafuta hayo si kubwa kama kwa majirani yake. Mapato ya mafuta ni 6% pekee za pato la taifa.

Viongozi wa ufalme wa Dubai wamefaulu kuweka msingi mpya wa uchumi katika biashara na utalii.

Viungo vya nje hariri