Dully Sykes
Abdul Sykes (alizaliwa 4 Desemba, 1980),[1] ni mwanamuziki wa Tanzania. Anakadiriwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa mwanzo wa muziki wa kizazi kipya Tanzania maarufu kama Bongo Flava.
Dully Sykes | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Abdul Sykes |
Pia anajulikana kama | Mr. Misifa |
Amezaliwa | 4 Desemba 1980 |
Asili yake | Tanzania |
Aina ya muziki | Hip hop R&B bongo Flava Pop |
Kazi yake | Mwimbaji Mtayarishaji wa muziki |
Wasifu
haririDully Sykes kama anavyojulikana kwa majina, Mr. Chicks au Mr. Misifa Ni mjukuu wa Abdulwahid Sykes, mwanaharakati wa kudai uhuru wa Tanganyika. Sykes Anajulikana kwa nyimbo zake maarufu zinatokana na matukio ya kweli kama Historia ya Kweli, Julieta, Leah, na Salome. Kufuatia kutolewa kwa albamu yake ya kwanza, Historia ya kweli, mwaka wa 2003.Sykes ameendelea kubaki katika chati za juu za muziki wa Tanzania akishirikiana na wasanii wakubwa wa muziki kutokea nchini Tanzania kama Harmonize na Marioo
Kili Music Awards
haririHizi ni tuzo alizoshiriki au kupokea kutoka Kili Music Awards katika misimu tofauti[2].
Mwaka | Mteule / kazi | Tuzo | Matokeo | |
---|---|---|---|---|
2012[3] | Bongo Flava | Alichaguliwa | ||
2012 | Bongo Flava | Wimbo bora wa Afropop | Alichaguliwa | |
2012 | Msanii bora wa kiume | Alichaguliwa | ||
2010 | Shikide | Wimbo bora wa Dancehall/Ragga | Alichaguliwa | |
2008 | Baby Candy | Wimbo bora wa Reggae/Ragga | Alichaguliwa | |
2007[4] | Dhahabu akiwa na Mr. Blue na Joslin | Wimbo bora wa ushirikiano | Alichaguliwa | |
2004 | Handsome | Albamu bora | Alichaguliwa | |
2012 | Maneno Maneno akiwa na Queen Darleen | Wimbo bora wa Dancehall/Ragga | Alishinda | |
2011 | Action akiwa na Ms. Triniti, CPWAA na Ngwair | Video Bora | Alishinda | |
2011 | Action | Wimbo bora wa Dancehall/Ragga | Alishinda |
Marejeo
hariri- ↑ Madenge (2021-08-18). "Quick Snapshot: Tanzanian Musician Dully Sykes". UnitedRepublicofTanzania.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
- ↑ "Kilitime". web.archive.org. 2004-12-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-12-04. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
- ↑ "Kili awards 2012 Nominees hawa hapa! – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
- ↑ "Kilitime". web.archive.org. 2011-07-13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-13. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dully Sykes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |