Queen Darleen

Mwanamuziki wa Tanzania

Mwanahawa Abdul Juma (amezaliwa 4 Novemba 1985) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania.

Queen Darleen
Queen Darleen akiwa ameshika tuzo ya "Kili" baada ya kuibuka mshindi wa tuzo hizo kwa wimbo bora mwaka 2012.
Queen Darleen akiwa ameshika tuzo ya "Kili" baada ya kuibuka mshindi wa tuzo hizo kwa wimbo bora mwaka 2012.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Mwanahawa Abdul Juma
Amezaliwa 4 Novemba 1985 (1985-11-04) (umri 38)
Asili yake Kigoma,Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava,Afro Pop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi
Ala sauti
Miaka ya kazi 2001–mpaka sasa
Studio Wasafi Records
Ame/Wameshirikiana na Dully Sykes, Inspector Haroun, Ali Kiba, Shilole, Rayvanny, Diamond Platnumz, Harmonize, Lavalava (mwanamuziki), Mbosso, Rich Mavoko

Queen alianza muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiwa ameshirikishwa na Dully Sykes katika wimbo wake wa Historia ya Kweli au maarufu Sharifa na Mtoto wa Geti Kali wa Inspector Haroun kabla kwenda kufanya muziki wa kujitegemea na 2006 kutoka kibao cha "Wajua Nakupenda alichofanya na Ali Kiba chini ya utayarishaji wake KGT na usimamizi wa DJ Guru Ramadhani. Mwaka wa 2012 alishinda tuzo ya Kili kwa wimbo bora wa Ragga/Dancehall.[1]

Baada ya harakati za muda mrefu, hatimaye amesainiwa na lebo ya WCB Wasafi iliyo chini ya Diamond Platnumz ambaye ni ndugu yake wa damu kwa upande wa baba.[2] Akiwa na WCB ametoa wimbo wake wa kwanza Kijuso uliotoka rasmi tarehe 17 Februari 2017 aliofanya na Rayvanny.[3] Halafu Ntakufilisi (Novemba 9 2017[4]), na Touch (22 Novemba 2017[5]). Vilevile alishiriki kuimba katika wimbo wa pamoja wa WCB Zilipendwa ulitoka tarehe 25 Agosti 2017.

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Queen Darleen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.