Dutwa
Dutwa ni kata na tarafa ya Wilaya ya Bariadi katika Mkoa wa Simiyu, Tanzania, yenye postikodi namba 39117 [1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 29,519 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,792 waishio humo.
Historia
haririEneo la tarafa ya Dutwa lilikuwa utemi katika tawala za jadi za jamii ya Wasukuma. Utemi huo ulianzishwa na ukoo wa Wahunda waliotokea kitongoji cha Bugunda, leo Wilaya ya Sikonge katika mkoa wa Tabora.
Mtemi wa kwanza aliitwa Gamaleka; mpaka sasa jumla ya watemi 27 wameshatawala Dutwa. Mtemi wa mwisho ni John Kasili. Orodha ya watemi ni kama ifuatavyo: Gamaleka, Sangulilu, Gambimeda, Mabera, Itobya, Nyasilu, Sagayika, Gilya, Balina, Lusha, Liswa, Galidi, Mushuda, Ileme, Buyunge, Mlola, Kasili, John.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 218
Kata za Wilaya ya Bariadi Vijijini – Mkoa wa Shinyanga - Tanzania | ||
---|---|---|
Banemhi | Dutwa | Gambosi | Gibishi | Gilya | Ihusi | Ikungulyabashashi | Itubukilo | Kasoli | Kilalo | Masewa | Matongo | Mwadobana | Mwasubuya | Mwaubingi | Mwaumatondo | Ngulyati | Nkindwabiye | Nkololo | Sakwe | Sapiwi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Simiyu bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |