Edna Adan Ismail

Mwanasiasa wa Somaliland

Edna Adan Ismail (alizaliwa 8 Septemba 1937) ni muuguzi mkunga, mwanaharakati na alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa mambo ya nje wa Somaliland[1] kuanzia mwaka 2003 hadi 2006. Aliwahi pia kuwa waziri wa mambo ya familia na maendeleo ya jamii.

Picha ya Edna Adan Ismail
Picha ya Edna Adan Ismail

Ni mkurugenzi na mwanzilishi wa hospitali ya Edna Adan Maternity Hospital huko Hargeisa na ni mwanaharakati na mwanzilishi wa mapambano kupinga ukeketaji. Pia ni raisi wa shirika la kuwasaidia waathirika wa mateso.[2]

Aliolewa na Mohamed Haji Ibrahim Egal aliyekuwa waziri mkuu wa Jimbo la Somaliland siku tano kabla ya Somalia kupata uhuru wake na baadaye akawa waziri mkuu wa Jamhuri ya Somalia mwaka (1960-1960) na (1967–69) na baadaye kuwa Raisi wa Somaliland mwaka (1993–2002).

Maisha ya awali hariri

 
Edna Adan Ismail akiwa na mtoto wa Chita mwaka 1968.

Edna Adan alizaliwa huko Hargeisa, (Somaliland ya waingereza) Tarehe 8 Septemba 1937,[3] binti wa daktari maarufu wa Somalia.[4] ni mmoja kati ya watoto watano kwa mama yake, lakini wawili walifariki wakati wa kuzaliwa. [5] Kwa nyakati hizo wanawake nchini Somaliland walikuwa hawaruhusiwi kupata elimu, lakini baba yake aliajiri mkufunzi kwaajili ya wavulana wa mtaani na yeye akapata nafasi ya kujifunza kusoma na kuandika pamoja nao. Baadae alienda shule huko Djibouti ambapo shangazi yake alikuwa ni mwalimu. Alipofikisha umri wa miaka nane, alikeketwa. Mipango ilipangwa na mama pamoja na bibi yake pale ambapo baba yake alikuwa kwenye safari ya kibiasha; aliporudi alikasirishwa sana kwa kitendo hicho.[5]

Kwa kutaka kuzuia wanawake wengine wasipitie mateso aliyoyapata, alijifunza uuguzi na ukunga nchini Uingereza katika chuo cha Borough Polytechnic, sasa hivi London South Bank University.[5] Baadae alifunga ndoa na Muhammad Haji Ibrahim Ega, mwanasiasa wa Somalia ambaye alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Somalia mwaka 1967.

Anatajwa kuwa msichana wa kwanza wa Somalia kusoma Uingereza,[6] Somaliland's first qualified nurse-midwife[6][7]

Marejeo hariri

  1. Gettleman, Jeffrey. "No Winner Seen in Somalia's Battle With Chaos", 2 June 2009. 
  2. "Somaliland's leading lady for women's rights: 'It is time for men to step up'", The Guardian, 23 June 2014. 
  3. Skaine, Rosemary (2008). Women Political Leaders in Africa. McFarlane. pp. 54. ISBN 9780786432998. 
  4. 125th Anniversary - Get Involved - My Cardiff. Cf.ac.uk. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-05-13. Iliwekwa mnamo 2021-07-22.
  5. 5.0 5.1 5.2 "Why giving birth in the U.S. is surprisingly deadly", National Geographic, 2018-12-13. 
  6. 6.0 6.1 Kristof, Nicholas D.; Sheryl WuDunn (2010). Half the Sky: Turning Oppression into Opportunity for Women Worldwide. Vintage Books. pp. 124–. ISBN 978-0-307-38709-7.  Unknown parameter |url-access= ignored (help)
  7. Somali Maternity Care Archived 14 Novemba 2012 at the Wayback Machine
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edna Adan Ismail kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.