Jibuti
Jibuti (Kifaransa: Djibouti; Kiarabu: جيبوتي), kirasmi Jamhuri ya Jibuti, ni nchi ndogo ya Afrika ya Mashariki kwenye Pembe la Afrika.
Jamhuri ya Jibuti | |
---|---|
جمهورية جيبوتي (Kiarabu) République de Djibouti (Kifaransa) Jamhuuriyadda Jabuuti (Kisomali) Gabuutih Ummuuno (Kiafar) | |
Kaulimbiu ya taifa: اتحاد، مساواة، سلام (Kiarabu) Unité, Égalité, Paix (Kifaransa) Midnimo, Sinnaan, Nabad (Kisomali) Inkittiino, Qeedala, Wagari (Kiafar) "Umoja, Usawa, Amani" | |
Wimbo wa taifa: Jibuti | |
Mahali pa Jibuti | |
Ramani ya Jibuti | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Jibuti |
Lugha rasmi | |
Lugha za taifa | |
Makabila (asilimia) | 60 Wasomali 35 Waafar 5 Waarabu |
Serikali | Jamhuri yenye mdikteta |
• Rais | Ismaïl Omar Guelleh |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 23 200[1] |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 976 143[1] |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 3.873[2] |
• Kwa kila mtu | USD 3 761[2] |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 7.193[2] |
• Kwa kila mtu | USD 6 985[2] |
Sarafu | Faranga ya Jibuti |
Majira ya saa | UTC+3 (Afrika Mashariki) |
Upande wa magari | Kulia |
Msimbo wa simu | +253 |
Msimbo wa ISO 3166 | DJ |
Jina la kikoa | .dj |
Imepakana na Eritrea, Ethiopia na Somalia upande wa bara. Kuna pwani ya Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden. Ng'ambo ya bahari iko nchi ya Yemen katika umbali wa km 20 pekee.
Jiografia
haririHali ya nchi inalingana kwa karibu na ile ya mataifa mengine katika Mashariki mwa Afrika, Jibuti ilipo, ikipakana na Ghuba ya Aden na Bahari ya Shamu, katikati ya Eritrea, Ethiopia na Somalia.
Eneo
haririKwa km 13 Jibuti inapakana na Eritrea, huku kukiwa na urefu wa kilomita 337 za mpaka kati ya Jibuti na Ethiopia, na mpaka wa km 58 na Somalia. Kwa jumla ina mpaka wa km 506. Pia ina pwani ya urefu wa km 314.
Jibuti inakaa kaika eneo la kufana, ikiwa karibu na leni zenye shughuli nyingi zaidi duniani la meli na pia karibu na mahali pa uchimbaji mafuta nchini Saudia.
Jibuti pia ni kituo cha reli ya Ethiopia-Jibuti.
Hali ya hewa
haririHali yake ya hewa ni ya joto kiasi, na pia haina mvua (ni jangwa).
Miinuko
haririMilima iliyopo katikati ya nchi hugawa tambarare za pwani kutoka plateau. Eneo la chini zaidi ni Ziwa Assal mita 155 chini ya usawa wa bahari na la juu zaidi ni volikano Moussa Ali yenye kimo cha mita 2028. Hakuna shamba la ukulima, unyunyizaji maji, mimea iliyojimeza huko (msitu upo tu katika milima ya Goda, hasa mbuga ya Day Forest). Takribani asilimia 9 ya nchi ni malisho yeliyojimeza (1993 mashariki). Kwa hiyo Jibuti inahesabiwa kuwa sehemu ya nyasi ya Ethiopia, isipokuwa kijisehemu kinachopakana na Bahari ya Shamu ambacho ni baadhi ya Jangwa la Pwani ya Eritrea ambayo inajulikana kuwa njia nzuri ya uhamiaji wa ndege ambao wanaweza kuwindwa[3].
Mazingira
haririMatukio ya kimaumbile ni pamoja na Matetemeko ya ardhi, kiangazi, mawimbi kutoka Bahari ya Hindi ambayo husababisha mafuriko na mvua kubwa. Malighafi ni pamoja na umeme kutoka ardhini (geothermal energy). Eneo hili limekumbwa na uhaba wa maji salama ya kunywa na pia kugeuka kwa eneo hilo kuwa jangwa.
Jibuti ni mwanachama wa makubaliano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ueneaji wa jangwa, viumbehai vilivyo hatarini, sheria ya bahari, kulinda ukanda wa ozoni na uharibifu wa mazingira na meli.
Historia
haririNchi ilikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Somalia ya Kifaransa, halafu (1967) Eneo la Kifaransa la Waafar na la Waisa, kutokana na majina ya makabila mawili makubwa zaidi ya eneo hilo.
Sababu ya kuanzishwa kwa koloni ilikuwa nia ya Ufaransa ya kuwa na bandari ya mji wa Jibuti karibu na Bab el Mandeb inayotawala mawasiliano kati ya Bahari Hindi na Bahari ya Shamu kuelekea Mfereji wa Suez.
Nchi ilipata uhuru tarehe 27 Juni 1977.
Hadi leo umuhimu na uchumi wake unategemea bandari, ambapo zinapitia asilimia 95 za bidhaa zinazoingizwa Ethiopia. Nchi hiyo imeunganishwa na Jibuti kwa reli, moja ya zamani, na nyingine mpya iliyokamilika mwaka 2016.
Watu
haririSiku hizi wakazi wengi (60%) ni Wasomali, hasa wa kabila la Waisa, halafu Waafar (35%). Asilimia 5 zilizobaki ni Waarabu, Waethiopia na Wazungu (hasa Wafaransa na Waitalia).
Lugha rasmi ni Kifaransa na Kiarabu. Kisomali na Kiafar ni lugha za taifa.
Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 94% za wakazi na ndio dini rasmi pekee. Asilimia 6 wanafuata Ukristo katika madhehebu mbalimbali, hasa Waorthodoksi wa Mashariki kutoka Ethiopia (3.2%), halafu Wakatoliki (1.4%) na Waprotestanti (chini ya 1%).
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "Djibouti". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2025). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) (Archived 2023 edition) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Djibouti)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 20 Oktoba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ http://www.worldwildlife.org/wildworld/profiles/terrestrial/at/at1304_full.html
Viungo vya nje
hariri- Serikali
- "Site Officiel de la République de Djibouti" (kwa Kifaransa). Serikali ya Jibuti.
{{cite web}}
: Unknown parameter|trans_title=
ignored (|trans-title=
suggested) (help) - "Office National de Tourisme de Djibouti". National Official of Tourism of Djibouti.
- Taarifa za jumla
- Djibouti entry at The World Factbook
- Djibouti profile from the BBC News.
- Jibuti katika Open Directory Project
- Mengineyo
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jibuti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |