Edward VI wa Uingereza
Edwad wa VI wa Uingereza (12 Oktoba 1537 - 6 Julai 1553) alikuwa mfalme wa Uingereza na Ireland kutoka tarehe 28 Januari 1547 mpaka kufa kwake.
Alipewa taji mnamo 20 Februari akiwa na umri wa miaka tisa. Edward alikuwa mtoto wa Henry VIII na Jane Seymour, na mfalme wa Uingereza wa kwanza kulelewa kama Mprotestanti.
Wakati wa utawala wake, eneo hilo lilikuwa chini ya uongozi wa Halmashauri ya Regency kwa sababu alikuwa hajafikia miaka ya kutosha. Baraza liliongozwa kwanza na Edward Seymour, Duke wa Somerset (1547-1549), na kisha na John Dudley.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Edward VI wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |