Henry VIII wa Uingereza

(Elekezwa kutoka Henry VIII)

Henry VIII (28 Juni 1491 – 28 Januari 1547) alikuwa mfalme wa Uingereza kuanzia tarehe 21 Aprili 1509 hadi kifo chake. Ni wa pili kutoka nasaba ya Tudor, akimfuata baba yake, Henry VII.

Mfalme Henri VIII alivyochorwa na Hans Holbein the Younger, Walker Art Gallery, Liverpool, Uingereza.

Maisha na matukio

hariri
Wake sita wa Henry VIII
(kufuatana na mwaka wa ndoa)
Anne Boleyn
(1533–1536)
Catherine Howard
(1540–1542)
Catherine Parr
(1543–1547)

Henry anajulikana hasa kwa kuoa wanawake sita, mmoja baada ya mwingine, na hasa kwa juhudi zake za kubatilisha ndoa yake ya kwanza na Katerina wa Aragona zilizomfanya hatimaye atenganishe Kanisa la Uingereza na Papa, akijifanya mkuu wa Kanisa. Pamoja na kutengwa na Kanisa Katoliki kwa sababu hiyo, aliendelea kusadiki mafundisho yake.[1]

Katika masuala ya ndani, Henry alijulikana kwa kubadilisha sana katiba ya nchi, akizidisha mamlaka yake mwenyewe. Waliopinga walishutumiwa kama wasaliti na mara nyingi kuhukumiwa adhabu ya kifo, akiwemo waziri mkuu Thomas More.

Matumizi yake yalikuwa makubwa mno, kwa ajili ya fahari na vita, hivi kwamba pesa nyingi alizofaulu kujipatia kwa kuteka mali ya monasteri na kuzuia kodi iliyokuwa inalipwa awali kwa Papa, hazikumtosha kamwe.

Aliunganisha Uingereza na Wales akawa pia mfalme wa kwanza wa Uingereza kushika nafasi ya mfalme wa Ireland.

Mwanzoni wengi walipendezwa naye[2], lakini baadaye alizidi kunenepa, afya yake ilitetereka, na hata nafsi yake ilivurugika na kumfanya mzinzi, mkatili, mwoga.[3]

Baada yake alitawala mwanae Edward VI.

Tanbihi

hariri
  1. Scarisbrick 1997, p. 361
  2. Guy 2000, p. 41.
  3. Ives 2006, pp. 28–36

Marejeo

hariri

Marejeo mengine

hariri

Maisha

hariri

Utafiti wa kitaalamu

hariri

Vyanzo

hariri

Viungo vya nje

hariri


  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Henry VIII wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.