Efeso (kwa Kigiriki Έφεσος) uliwahi kuwa moja kati ya majiji ya dunia, lakini kwa sasa halina wakazi.

Ramani ya Efeso.
Magofu ya Maktaba ya Chelso.
Magofu ya mahali pa maigizo pa Efeso.

Lilianzishwa na Wayunani huko Lidia kwenye mto Kaistro unapoishia katika Bahari ya Kati, kwenye pwani ya Uturuki wa leo.

Lilikuwa kituo kikubwa cha biashara na magofu yake ni kati ya mahali muhimu pa akiolojia.

Mtume Paulo aliishi huko miaka mitatu akawaandikia Wakristo wake barua muhimu.

Baadaye alihamia huko Mtume Yohane ambaye pia katika Kitabu cha Ufunuo aliandika barua kwa malaika wa Kanisa hilo pamoja na nyingine sita kwa malaika (maaskofu) wa Makanisa ya kandokando.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Efeso kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.