Chechele (Stenostiridae)

Ndege wadogo wa familia Stenostiridae
(Elekezwa kutoka Elminia)
Chechele
Chechele buluu
Chechele buluu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Stenostiridae (Ndege walio na mnasaba na chechele)
Ngazi za chini

Jenasi 4, spishi 9:

Chechele ni ndege wa familia Monarchidae na Stenostiridae. Zamani wale wa Stenostiridae waliainishwa katika familia Muscicapidae (Culicicapa), Monarchidae (Elminia), Sylviidae (Stenostira) na Rhipiduridae (Chelidorhynx), lakini uchunguzi wa ADN umeonyesha kwamba wana mnasaba na kwa hivyo wamepewa familia yao.

Wana rangi ya buluu (Elminia), ya kijivu (Stenostira) au ya manjano (Chelidorhynx na Culicicapa). Wanatokea misituni au porini kwa vichaka katika Afrika na Asia. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika panda ya matawi. Jike huyataga mayai 2.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri