Enea (Biblia)
Enea (kwa Kiingereza Aeneas) alikuwa mtu wa Palestina katika karne ya 1.
Kadiri ya Matendo ya Mitume 9:32-33, aliishi Lydda na alikuwa kiwete kwa muda wa miaka minane, lakini Mtume Petro alipomuambia, "Yesu Kristo anakuponya. Simama na chukua godoro lako"[1], mara alipona na kuinuka.
Ingawa kitabu hicho cha Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo hakisemi wazi, F. F. Bruce na wengineo wanadhani Enea alikuwa Mkristo tayari[2].
Simulizi la Enea linafuatwa na lile la ufufuko wa Tabita wa Yopa.
Tanbihi
hariri- ↑ Williams, David J. (2011). Acts. Understanding the Bible Commentary Series. Baker Books. uk. 166. ISBN 978-1-4412-3745-3.
- ↑ F. F. Bruce, Commentary on the Book of the Acts (Grand Rapids: Eerdmans, 1964), 210.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Enea (Biblia) kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |