Zuwanende
(Elekezwa kutoka Erithacus)
Zuwanende | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 5, spishi 13:
|
Zuwanende ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia ya Muscicapidae. Ndege hawa wana mnasaba na kurumbiza lakini mkia wao ni mfupi zaidi na domo ni jembamba. Wana rangi ya kahawa au zaituni mgongoni na koo na kidari ina rangi ya machungwa pengine karibu na nyekundu pengine njano. Hawa ni ndege wa misitu ya Afrika kusini kwa Sahara, kwa kawaida milimani, isipokuwa zuwanende wa Ulaya. Hula wadudu, buibui na nyungunyungu, pengine beri na mbegu pia. Hujenga tago lao katika tundu ya asili na jike huyataga mayai 2-6.
Spishi za Afrika
hariri- Erithacus rubecula, Zuwanende wa Ulaya au Mkesha Mwekundu (European Robin)
- Erithacus r. rubecula, Zuwanende wa Ulaya
- Erithacus r. superbus, Zuwanende wa Kanari (Canary Islands Robin)
- Erithacus r. witherbyi, Zuwanende Kaskazi (West African Robin)
- Pogonocichla stellata, Zuwanende Kidari-njano (White-starred Robin)
- Sheppardia aequatorialis, Zuwanende Mashavu-kijivu (Equatorial Akalat)
- Sheppardia aurantiithorax, Zuwanende wa Rubeho (Rubeho Akalat)
- Sheppardia bocagei, Zuwanende Mashavu-mekundu (Bocage's Akalat)
- Sheppardia cyornithopsis, Zuwanende Mbavu-nyekundu (Lowland Akalat)
- Sheppardia gabela, Zuwanende wa Gabela (Gabela Akalat)
- Sheppardia gunningi, Zuwanende-pwani (East Coast Akalat)
- Sheppardia lowei, Zuwanende wa Iringa (Iringa Akalat)
- Sheppardia montana, Zuwanende wa Usambara (Usambara Akalat)
- Sheppardia sharpei, Zuwanende Mashavu-kahawia (Sharpe's Akalat)
- Stiphrornis erythrothorax, Zuwanende-misitu (Forest Robin)
- Swynnertonia swynnertoni, Zuwanende baka-jeupe (Swynnerton's Robin)
Picha
hariri-
Zuwanende wa Ulaya
-
Zuwanende mashavu-kijivu
-
Zuwanende-misitu
-
Zuwanende baka-jeupe