Eugenia E. Ravasio
Eugenia Elisabetta Ravasio (Capriato San Gervasio, Bergamo, Italia, 4 Septemba 1907 - Anzio, Lazio, 10 Agosti 1990) alikuwa Mkuu wa shirika la Masista Wamisionari wa Mama yetu wa Mitume kuanzia mwaka 1935 hadi mwaka 1947.
Urithi wake muhimu zaidi ni ujumbe kutoka kwa Mungu Baba Mwenyezi “Baba huwaambia watoto wake"[1], ufunuo pekee ulioletwa na Mungu na kutambuliwa na Kanisa kama mafundisho sahihi, baada ya miaka kumi ya utafiti. Ni jambo muhimu kuwa mnamo mwaka 1932 Baba Mungu alitoa ujumbe huo kwa Mama Eugenia na kuuweka katika Kilatini, lugha ambayo haikujulikana kabisa kwake.
Maisha
haririMama Eugenia alizaliwa katika familia ya wakulima akapata elimu ya msingi tu, kwa sababu akiwa kijana ugonjwa wa mama yake wa muda mrefu ulimlazimu kubaki nyumbani na kujishughulisha na kazi za nyumbani hivyo kushindwa kwenda shuleni mara nyingi.
Baada ya kufanya kazi ya ufumaji kwa miaka kadhaa katika kiwanda, alijiunga na shirika la masista wamisionari wa Mama yetu wa Mitume, akiwa na miaka 20. Alichaguliwa kama Mama Mkuu wa shirika akiwa na umri wa miaka 27.
Kwa kutambua mchango wake kwa jamii, nchi ya Ufaransa ilimtunuku heshima ya mtumishi bora katika jamii (Couronne Civique) ikiwa ni heshima ya juu katika utumishi wa umma uliotukuka.
Mafanikio mengine
haririTangu mwanzo wa maisha yake ya kitawa, sista huyo alikuwa amevutia wakurugenzi wake kwa sababu ya uchaji wake Mungu, utii wake, unyenyekevu na na mwenendo mzuri wa mfano. Wakati wa miaka kumi na mbili ya shughuli za umishonari alianzisha vituo zaidi ya 70 - kila vyao chenye nyumba ya wagonjwa/nyumba ya dawa, shule na kanisa - katika sehemu za mbali zaidi za Afrika, Asia na Ulaya. Aligundua dawa ya kwanza dhidi ya ukoma, iliyotengenezwa kwa kutumia mbegu ya mmea wa kitropiki. Wakati wa kipindi cha 1939-41 alitunga, akaendeleza na kutimiza dhana ya "Jiji la Wenye Ukoma" huko Azopte (Kodivaa ). Hiyo ilikuwa kituo kikubwa, chenye eneo la mita ya mraba 200, kwa ajili ya wa wagonjwa wenye ukoma.
Ujumbe wa Baba - " Baba huwaambia watoto wake"
haririLengo lake sahihi ni kumwezesha Mungu Baba awe maarufu na aheshimiwe, hasa kwa kuanzisha karamu maalum iliyotarajiwa na Kanisa. Lengo lake Sikukuu hiyo maalum ilikuwa ya kuimarisha, kwa upya mambo ya roho baina ya Wakristo wengi na, licha yake, ya kuwaelekeza mwongozo wa Mungu Mwokozi: "Kila kitu unachomwomba Baba kwa niaba yangu ..." na tena " Utaomba hivyo: 'Baba yetu ...' ”. Isitoshe Sikukuu hiyo ya liturujia kwa kusudi jema Mungu Baba ilikuwa na lengo la kumwinuea macho yetu yule ambaye aliitwa na mtume Mtakatifu Yakobo "Baba wa mianga, ambaye kila kutoa kuliko kwema hushuka kwake ,...". Kwa ajili yake roho zitazoea kuzingatia uzuri wa Mungu na maongozi yake Baba. Wangetambua kwamba maongozi haya ni kweli ya Mungu Utatu Mtakatifu, na kwamba ni kwa sababu ya asili yake ya Kimungu, ya wote wa Utatu Mtakatifu, kwamba Mungu hueneza duniani hazina yake isiyoelezeka ya huruma Yake isiyo na kikomo. Ujumbe hueleza kwamba elimu ya Baba, ni lazima iangaliwe kwa upya, kusomwa kwa bidii na kujaribiwa katika maisha.
Tanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |