Archaea
Halobacteria sp. strain NRC-1, kila seli ina urefu wa µm 5
Halobacteria sp. strain NRC-1,
kila seli ina urefu wa µm 5
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Archaea
Woese, Kandler & Wheelis, 1990
Ngazi za chini

Himaya 3, faila za juu 2:

Archaea (tamka arkea; kutoka Kigiriki ἀρχαῖος, archaĩos, „kizee sana, kiasili“) ni kundi la vidubini vyenye seli moja tu.

Muundo wa seli zao una tabia za pekee, hivyo uainishaji wa kisayansi hauzipangi pamoja na bakteria, bali katika domeni ya pekee, ambayo ni domeni ya tatu ya uhai pamoja na bakteria na Eukaryota. Siku hizi eukaryota zinachukuliwa kuwa zimetokana na kuingizwa kwa seli za bakteria ndani ya seli ya archaea. Seli hizi za bakteria zikawa mitokondrio (pia dutuvuo). Mhenga wa mimea alipata seli nyingine za bakteria, ambazo zikawa kloroplasti. Hii inadokeza kwamba eukaryota ni aina za juu za archaea.

Archaea hazikujulikana kwa muda mrefu kwa sababu zinaonekana kwa hadubini tu. Mwili wote ni seli moja tu. Kimaumbile zinafanana na bakteria, hivyo kwa muda mrefu zilitazamwa kama kundi la bakteria.

Archaea zilitambuliwa tangu 1977 kama kundi la pekee. Ilionekana ya kwamba kemia ndani ya seli ni tofauti. Zina uwezo wa kutumia mata nyingi kama lishe kushinda bakteria au eukaryota.

Zimepatikana katika mazingira magumu pasipo viumbehai wengine

Kwa hiyo zimepatikana ndani ya chemchemi ya maji moto na maziwa ya chumvi au magadi. Ziko mazingira pasipo na oksijeni na pia ndani ya utumbo wa binadamu.

Archaea ni sehemu muhimu ya planktoni.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Archaea kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.