Fadlu Davids
Fadluraghman, alimaarufu Fadlu Davids (alizaliwa 21 Mei 1981 huko Cape Town, Western Cape) ni mchezaji mstaafu wa Afrika Kusini wa soka mshambuliaji ambaye alicheza katika klabu ya ligi kuu ya Premier Soccer League ya Maritzburg United kabla ya kustaafu kwake.[1] Alikuwa mfungaji bora mara mbili katika Ligi ya Kwanza ya Taifa ya Afrika Kusini.
Tangu kustaafu kwake mwaka 2012, Davids amehudumu kama kocha msaidizi wa Ernst Middendorp katika Maritzburg United. Wakati Middendorp alipoondoka Martizburg United mwaka 2016, Davids aliteuliwa kuwa kocha wa muda wa Maritzburg kwa mara ya tatu katika kazi yake. Ndugu yake, Maahier Davids, aliteuliwa kuwa msaidizi wake.[2]
Baada ya kuwasili kwa Roger De Sá, Davids alirejea katika nafasi yake kama kocha msaidizi wa Maritzburg. Hata hivyo, baada ya mechi saba tu, alirudia nafasi yake kama kocha wa muda baada ya De Sá kujiuzulu.[onesha uthibitisho] Davids alikuwa kaimu kocha kwa muda wote wa 2016–17 South African Premier Division. Tarehe 1 Julai, Maritzburg United ilitangaza kuwa Fadlu Davids angekuwa kocha wa kudumu baada ya kuonyesha uwezo mzuri akiwa kaimu kocha; alikuwa anahusika katika mechi tisa za mwisho wa msimu, akishinda nne, sare tatu, na kupoteza mbili. Msimu wa kwanza kabisa wa Davids kama kocha timu haikua na mafanikio, Ilipata pointi 4 tuu kwenye mashindano ya kufuzu 2018–19 CAF Confederation Cup na pia walifungwa katika fainali za 2017–18 Nedbank Cup, ambapo ilikuwa nafasi yao ya mwisho ya kufuzu kwa mashindano ya CAF. Timu ya Davids ilicheza mechi 15 za ligi na kushinda mara moja tu, na tarehe 24 Desemba, Maritzburg United ilimfuta kazi Davids. Davids alirudi kuwa kocha msaidizi, wakati huu kwa Orlando Pirates F.C., na amekuwa katika nafasi hiyo tangu tarehe 15 Januari 2019."
Davids alijijengea sifa ya kuendeleza wachezaji vijana baada ya kutoa fursa kwa wachezaji kama vile Siphesihle Ndlovu, Bandile Shandu, na Mlondi Dlamini, ambao wote walikuwa awali ni wavulana wa mipira.[3]
- Ajiunga na Maritzburg United: 2007
- Vilabu vya awali: Silver Stars; Vasco Da Gama; Manning Rangers; Santos Cape Town; Chernomorets Burgas, Bulgaria; Avendale Athletico, Mother City
Marejeo
hariri- ↑ "Davids joins coach's staff", News24. (en)
- ↑ www.realnet.co.uk. "Fadlu Davids takes charge yet again at Maritzburg United". Retrieved on 2023-06-10. Archived from the original on 2016-12-26.
- ↑ Ngidi, Njabulo. "Perennial caretaker Davids did in three games what predecessor Sa couldn't do in seven outings". Times LIVE. Iliwekwa mnamo 2017-05-09.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fadlu Davids kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |