Faridi
Faridi (ar., lat. & ing. Alphard pia α Alfa Hydrae [1], kifupi Alfa Hya, α Hya) ni nyota angavu zaidi katika makundinyota ya Shuja (Hydra) na nyota angavu ya 49 kwenye anga ya usiku.
(Alfa Hydrae, Alphard) | |
---|---|
Kundinyota | Shuja (Hydra) |
Mwangaza unaonekana | 2.0 |
Kundi la spektra | K3 II-III |
Paralaksi (mas) | 18.40 ± 0.78 |
Umbali (miakanuru) | 177 |
Mwangaza halisi | -1.69 |
Masi M☉ | 3 |
Nusukipenyo R☉ | 50 - 56 |
Mng’aro L☉ | 780 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 4120 |
Majina mbadala | Alfard, Alphart, Cor Hydrae, 30 Hydrae, HR 3748, BD−08° 2680, HD 81797, SAO 136871, FK5 354, HIP 46390. |
Jina
Faridi inayomaanisha “pweke” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الفرد al-fard inayomaanisha „ peke yake " kwa sababu hakuna nyota ng’avu nyingine iliyo karibu. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Alphard" [3] .
Alfa Hydrae ni jina la Bayer kwa sababu Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki na Faridini nyota angavu zaidi katika Shuja - Hydra.
Tabia
Faridi iko kwa umbali wa miakanuru takriban 420 kutoka Jua letu. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 2 na mwangaza halisi ni -1.69. Masi ni Mo 3 , nusukipenyo Ro 50 – 56 [4]. Spektra yake ni ya aina ya K3[5]. "K" inamaanisha ni nyota iliyoondoka tayari kwenye safu kuu na sasa imekuwa jitu jekundu iliyopanuka kuwa na nusukipenyo mara 50 za Jua letu. Hivyo mng’aro wake ni kali vilevile ikiwa na Lo 780[6].
Faridi inazunguka polepole kwenye mhimili wake katika muda wa miaka 2.4 [7].
Tanbihi
- ↑ Hydrae ni uhusika milikishi (en:genitive) wa "Hydra" katika lugha ya Kilatini na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa, Beta, Gamma Hydrae, nk.
- ↑ ling. Knappert 1993
- ↑ Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
- ↑ da Silva (2006); makadirio ya da Silva na Piau yanatofautiana kuhusu masi
- ↑ Piau, L.; et al. (February 2011), (HD 81797)
- ↑ Piau, L.; et al. (February 2011), (HD 81797)
- ↑ Kaler, ALPHARD (Alfa Hydrae)
Viungo vya Nje
- Constellation Guide:Hydra
- Hydra, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
- ALPHARD (Alfa Hydrae), kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Marejeo
- Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
- Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
- Piau, L.; et al. (February 2011), "Surface convection and red-giant radius measurements", Astronomy and Astrophysics, 526: A100 online hapa
- da Silva, L.; et al. (November 2006). "Basic physical parameters of a selected sample of evolved stars". Astronomy and Astrophysics. 458 (2): 609–623. online hapa