Felix Chemonges (alizaliwa 10 Oktoba 1995)[1][2] ni mwanariadha wa mbio ndefu kutoka Uganda.

Mwaka 2018, alishiriki katika mbio za nusu marathoni za wanaume katika Mashindano ya Dunia ya Nusu ya Marathon ya IAAF ya mwaka 2018 yaliyofanyika Valencia, Uhispania. Alimaliza katika nafasi ya 26.[2] Mnamo Novemba Felix alicheza kwa mara ya kwanza katika mbio za marathon akishika nafasi ya pili kwa saa 2:11:57 katika mbio za Beirut Marathon.

Mwaka 2019, Chemonges alishika nafasi ya pili katika Mbio za Borealis Linz Donau Marathon nchini Austria akitumia saa 2:09:19. Rekodi ya Kitaifa ya Uganda muda wa 2:05:12.

Mwaka 2020, Chemonges alishiriki katika mbio za 76 za ziwa Biwa Mainichi Marathon ambapo alimaliza wa 9 kwa saa 2:10:08.

Mwaka 2021, Chemonges alishiriki katika mbio za NN Mission Marathon huko Enschede, Uholanzi, ambapo alimaliza wa 8 kwa saa 2:09:59.[3] Mbio hizo zilishindwa na Mkenya Eliud Kipchoge. Chemonges alichaguliwa kujiunga na wenzake Stephen Kiprotich na Fred Musobo kwenye timu ya Uganda ya marathon ya wanaume katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020. [4]

Marejeo

hariri
  1. "Felix Chemonges".
  2. 2.0 2.1 "Men's Results" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-09. Iliwekwa mnamo 2024-11-15.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  3. "Filex CHEMONGES | Profile | World Athletics".
  4. "OLYMPICS: Kiprotich picked for Uganda marathon team".
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Felix Chemonges kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.