Five Years Gone
"Five Years Gone" ni sehemu ya ishirini ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Hiki ni kipengele cha mwisho kabla ya vipande vitatu vya mwisho vya msimu wa kwanza. Sehemu hii awali ilijulikana kama "String Theory." Jina lilibadilishwa na kuwa "Five Years Gone", na "String Theory" ilitumika kama jina la Ukurasa wa 30 kwenye riwaya za picha za Heroes. [1]
"Five Years Gone" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
Hiro wa Baadaye anaelezea kuhusu mustakabalis. | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 1 Sehemu 20 | ||||||
Imetungwa na | Joe Pokaski | ||||||
Imeongozwa na | Paul Edwards | ||||||
Tayarisho la | 120 | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | 30 Aprili 2007 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
| |||||||
Orodha ya sehemu za Heroes |
Hadithi
haririSehemu hii inahusu hasa juu ya Hiro Nakamura na Ando Masahashi wakisafiri miaka mitano baadaye, inaonesha mahali dunia itakapokuwa iwapo mlipuko wa bomu hautozuiwa. Hiro wa Baadaye, mara iliyopita alivamia kwenye kipengele cha "Hiros", kipengele maarufu sana, wakati huu amekuwa kama gaidi mkubwa wa dunia na mkuu wa Battōjutsu. Ando aliuawa kwenye mlipuko, ambapo kwa mujibu wa Peter, hiyo ndiyo sababu Hiro amepoteza upande wake wa uchale na kuwa na uchungu wa kubadilisha yaliyopita.
Nathan Petrelli kwa sasa ni Rais wa Marekani, na Mohinder Suresh akiwa kama Mshauri Mkuu wa Masuala ya Afya na Matt Parkman akiwa kama Mkuu wa Usalama wa Taifa akiwa na Haitian ubavuni kwake. Niki Sanders amekuwa menenguaji tena, anajiita "Jessica", jina la alter ego wake wa zamani na dada'ke, ikiwa kama jina la kisanii. Mtoto wake Micah aliuawa kwenye mlipuko ambao umeharibu kwa kiasi kikubwa mji wa New York. Niki ana uhusiano wa kimapenzi na Peter Petrelli, ambaye ana kovu la shavu lisilioonekana vizuri katika upande wa shavu la kushoto.[2]
Marejeo
hariri- ↑ TV Recap: Heroes - Chapter 20 - Five Years Gone
- ↑ "String Theory". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-04-30. Iliwekwa mnamo 2007-03-26.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|1=
(help)
Viungo vya Nje
hariri- "Five Years Gone" at the Internet Movie Database
- "Five Years Gone" at TV.com
- Beaming Beeman: Episode 20: Five Years Gone, Director's blog on the filming of this episode.