Francesco Coccopalmerio
Francesco Coccopalmerio (alizaliwa 6 Machi 1938) ni kardinali wa Italia.
Alikuwa rais wa Baraza la Kipapa la Matini ya Sheria za Kanisa kuanzia alipoteuliwa na Papa Benedikto XVI tarehe 15 Februari 2007 hadi Papa Fransisko alipopokea ombi lake la kustaafu tarehe 7 Aprili 2018.
Alianza huduma yake katika Jimbo Kuu la Milano akateuliwa kuwa askofu msaidizi mwaka 1993. Mwaka 2000, alihamia kwenye Curia ya Roma.[1]
Marejeo
hariri- ↑ "Opus Dei down to one top Vatican official; Benedict's ties to Communion and Liberation deepen", National Catholic Reporter, 16 February 2007.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |