Frank Chester Robertson

mwandishi wa mashairi(1890-1969)

Frank Chester Robertson (azaliwa 12 Januari 1890 - alifariki 29 Julai 1969) ni mwandishi wa Marekani aliyejulikana kwa kazi za riwaya za magharibi zilizofanyika mwishoni mwa karne ya 18 na mwishoni mwa karne ya 19. Alichapisha makala za vitabu zaidi ya 150 na makala nyingi za stori fupi fupi pamoja na mfululizo wa makala za magazeti. Kwa miaka ya baadae aliweza kuandika kwa mpangilio katika gazeti la Provo Herald lililoitwa "The Chopping Block".

Maisha ya Awali

hariri

Robertson alizaliwa katika mji wa Idaho. Baba yake alikuwa ameokoka katika kanisa la Yesu kristo la watakatifu wa siku za mwisho (Wamormoni) na kuhamisha familia yake hadi Chesterfield, Idaho. Familia yake walikuwa wakulima ili kuisaidia familia yake alichunga kondoo na mama yake alihudumu kama mfanyakazi wa posta kwa muda kipindi baba yake akiwa kwenye misheni ya LDS Robertson [1]. Mnamo mwaka 1914 aliweza kupata hekari 320 (kilomita za mraba 1.3) nyumbani karibu na vilima vilivyopo maili chache kutokea mashariki ya Chesterfied.

Marejeo

hariri
  1. www.bibliopolis.com. "A Ram in the Thicket.; The story of a roaming homesteader family on the Mormon frontier by Frank C. Robertson on Benchmark Books". Benchmark Books (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-07-19.