Wamormoni ni kundi la watu wanaohusiana na dini ya Mormoni, iliyoanzishwa na Joseph Smith huko New York, Marekani, katika miaka ya 1820 akidai alipata njozi na kuonyeshwa kitabu kitakatifu.

Kioo cha rangi kikionyesha njozi ya kwanza ya Joseph Smith.

Baada ya kifo chake (1844), Wamormoni walimfuata Brigham Young hadi eneo la Utah.

Leo wengi wao ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku ya Mwisho (kifupisho cha Kiingereza LDS Church).

Kiini cha utamaduni wao ni jimbo la Utah, ambapo wao ndio wengi kati ya wakazi wote, lakini siku hizi Wamormoni wanaoishi nchini Marekani ni wachache kuliko wanaoishi nje kutokana na umisionari mkubwa wanaoufanya duniani kote.

Idadi yao inakadiriwa kuwa milioni 15.

Imani yao hariri

 
Mpango wa Wokovu.

Wamormoni wanasadiki Biblia pamoja na maandishi mengine kama vile Kitabu cha Mormoni.

Wanasisitiza sharti la kumfuata Yesu Kristo ili kumrudia Mungu, pamoja na kupata ubatizo.

Wamormoni wanajiita Wakristo, ingawa mafundisho yao mbalimbali ni tofauti na yale ya madhehebu yote ya Ukristo, kiasi cha kutokubaliwa nayo (k.mf. Kanisa Katoliki halitambui ubatizo wao, hivyo linawahesabu kama dini tofauti).

Maadili hariri

Pamoja na kukubali mitara kwa msingi wa Agano la Kale, Wamormoni wana maadili imara upande wa jinsia (wakipinga uasherati, uzinifu na ushoga) na wa matumizi ya mwili (vileo, tumbaku, kahawa, chai n.k.).

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.