Fu-Gee-La
"Fu-Gee-La" ni single ya kwanza kutoka katika albamu ya pili ya kundi zima la The Fugees', The Score. Wimbo, ambao ulitayarishwa na Salaam Remi, imemjulisha samupuli ya wimbo wa "If Loving You Is Wrong, I Don't Want To Be Right" wa Ramsey Lewis, na kiitikio chake kinatokana na "Ooh La La La" wa Teena Marie. Maremixi kadhaa ya wimbo yalifanyika ("Refugee Camp Remix" na "Sly & Robbie Remix", ambayo pia imemshirikisha Akon wakati yu bwana mdogo) pia ameonekana kwenye The Score. Hii ni single pekee ya The Fugees kupata mauzo ya hali ya juu, na ilitunukiwa dhahabu na RIAA.[1]
“Fu-Gee-La” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Fugees kutoka katika albamu ya The Score | |||||
Imetolewa | 9 Januari 1996 | ||||
Muundo | 12" single | ||||
Imerekodiwa | 1995 | ||||
Aina | Hip hop, Rap | ||||
Urefu | 4:20 | ||||
Studio | Ruffhouse Records | ||||
Mtunzi | Nelust Wyclef Jean Samuel Prakazrel Michel Lauryn Noel Hill Allen McGrier Teena Marie Salaam Remi | ||||
Mtayarishaji | Salaam Remi | ||||
Certification | Gold (RIAA) | ||||
Mwenendo wa single za Fugees | |||||
|
Muziki wa video
haririMuziki wa video wa Fu-Gee-La ulipigwa nchini Jamaika. Muziki wa video unaelezea kisa kinachohusiana na masuala ya wizi wa mapesa, ambamo kila mmoja kwenye kundi hili kachukua nafasi yake husika. Mwanzoni anaonekana Pras akishuka kwenye pikipiki na mali ya magendo. Wakati huohuo anaoneshwa Hill akivizia askari apite ili aweze kupora mzigo uliokuwa karibu naye. Mbeleni, anaonekana Jean akiwa mbioni na mwishowe wote wanakutana mahala pamoja na kuanza mbio za magari baina ya polisi na kina Fugees. Mbio zile ziliishia kivukoni ambapo kina Hill wamechelewa kufika pale kwa sababu wale mapolisi walipita njia ya mkato na kutangulia kufika kabla ya wao. Kilichofuata ni kumwaga mapesa wale mapolisi wasishughulike na wao halafu wanaonekana wakirukia boti lililokuwa likiondoka kivukoni taratibu.
Orodha ya nyimbo
haririCD1
hariri- "Fu-Gee-La" (Album Version) (4:15)
- "Fu-Gee-La" (North Side Mix) (4:15)
- "Fu-Gee-La" (Refugee Camp Remix) (4:24)
- "Fu-Gee-La" (Sly & Robbie Mix) (5:33)
- "Fu-Gee-La" (Wyclef's Global Acoustic Mix) (4:18)
- "Fu-Gee-La" (Fugi Acapella) (4:08)
CD2
hariri- "Fu-Gee-La" (Album Version) (4:15)
- "Fu-Gee-La" (Refugee Camp Remix Instrumental) (4:22)
- "How Many Mics" (4:22)
- "How Many Mics" (Acapella) (4:16)
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-08. Iliwekwa mnamo 2010-06-09.