Prakazrel Samuel Michel, anajulikana kama Pras, (amezaliwa tar. 19 Oktoba 1972) ni mshindi wa Tuzo ya Grammy (Grammy Award) akiwa kama rapa, mwigizaji na mtayarishaji bora wa muziki kutoka nchini Marekani. Pras vilevile ni mmoja kati ya wanakundi la muziki wa hip hop maarufu kama The Fugees, ni miongoni mwa makundi yaliyofikiriwa kuwa yalipata sifa kubwa sana kwenye miaka ya 1990, kwa kutoa albamu ya The Score iliyofanya vizuri katika soko la muziki.

Pras
Jina la kuzaliwa Prakazrel Samuel Michel
Amezaliwa 19 Oktoba 1972 (1972-10-19) (umri 52)
Aina ya muziki Hip hop, Alternative hip hop, Soul, neo-soul, R&B, Reggae, Folk
Kazi yake Rapa, Mtayarishajir, Mpangiliaji, Mtunzi wa nyimbo
Miaka ya kazi 1993–mpaka sasa
Studio Columbia, Ruffhouse
Ame/Wameshirikiana na Fugees, Refugee Camp All-Stars
Pras (2015)

Wasifu

hariri

Maisha ya awali

hariri

Pras alizaliwa mjini Haiti na kukulia mjini Brooklyn,New York na South Orange, New Jersey, Pras ni mkulima wa muziki toka awali. Akiwa na umri wa maiaka kumi na tatu, Pras alikutana na Lauryn Hill akiwa na umri wa miaka 12, Lauryn ni mwimbaji aliye na kipaji na sauti nzuri, Pras aliligundua hilo mwanzo tu wa kukutana nae. Mnamo mwaka wa 1988, Pras alimtamblisha Lauryn kwa "binamu yake", Wyclef Jean, na baadae wakaja kuunda kundi la muziki liloitwa Tranzlator Crew. Kundi baadae lilibadilshwa jina na kuitwa The Fugees, kama kumbu kumbu kwa wakimbizi wa Haiti waliotelekezwa katika kutaka kupita katika bahari ya Marekani.

Albamu alizotoa

hariri

Albamu za peke yake

hariri
  • 1998: Ghetto Supastar
  • 2005: Win Lose or Draw
  • 2008: Experience Magic

Nyimbo za moja moja za peke yake

hariri
  • 1998: "Ghetto Supastar (That Is What You Are)" (featuring Ol' Dirty Bastard & Mýa)
  • 1998: "Blue Angels"
  • 1998: "Another One Bites the Dust" (Queen featuring Wyclef Jean, Pras & Free)
  • 1999: "What'cha Wanna Do" (featuring The Product & Free)
  • 1999: "Avenues" (featuring Refugee Camp Allstars)
  • 2001: "Miss California" (Dante Thomas featuring Pras)
  • 2005: "Haven't Found"
  • 2007: "Turn You On" (DeDe featuring Pras)
  • 2007: "Pop Life from the soon to be released CD [ Experience Magic]

Shughuli za uigizaji na utaarishaji

hariri
  • Mystery Men (1999) - Tony C (credited as Prakazrel Michel)
  • Turn It Up (2000)- Denzel/Diamond (credited as Pras Michel) (co-producer)
  • Higher Ed (2001)- Ed Green (credited as Pras Michel) (executive producer)
  • Go For Broke (2002)- Jackson/Jackie (credited as Pras Michel) (producer)
  • Nora's Hair Salon (2004)
  • Careful What You Wish For (2004) - Zen Salesman (credited as Pras Michel)
  • Feel The Noise (2007) - Electric
  • First Night (2006) - himself (producer)
  • The Mutant Chronicles (2007)- Captain Michaels (producer)

Viungo vya Nje

hariri