Gneiss

(Elekezwa kutoka Gneis)

Gneis (pia "gneiss") ni aina ya mwamba metamofia inayopatikana kwa wingi duniani. Asili yake ni miamba mashapo (sedimentary rocks) na pia miamba ya mgando (igneous rocks) iliyoathiriwa na joto pamoja na shinikizo kubwa kwa miaka mingi.[1]

Mwamba wa Gneiss mara nyingi huonyesha milia ya rangi tofauti.
Gneis iliyoundwa na metamofia ya itale.

Jina la gneis / gneiss lina asili ya Kijerumani ambapo inamaanisha kitu kinachong'aa, maana wakati mwingine kuna fuwele vimeto ndani yake[2].

Miamba ya gneis kwa kawaida huonekana kuwa na milia ya madini yenye rangi tofauti. Ilitokea katika vilindi vya ardhi ambako ilishinikizwa na uzito mkubwa wa miamba juu yake. Katika hali hiyo mwamba si imara lakini kinamo. Miendo katika ganda la dunia huvuta na kusukuma mwamba kinamo na hapo madini ndani ya mwamba huanza kuachana kiasi na kuganda tena kwa matabaka ya pekee yanayoonekana kama milia ya gneis[3].

Marejeo

hariri
  1. Blatt, Harvey, Robert J. Tracy & Ernest G Ehlers 1996. Petrology : igneous, sedimentary, and metamorphic. Freeman, New York.
  2. Harper, Online Etym. Dict., "gneiss"; "gneis" ni tahajia ya Kijerumani ya kisasa, "gneiss" ni tahajia ya kale iliyopokewa katika Kiingereza
  3. Marshak, Stephen (2013). Essentials of Geology (4th ed.). W.W. Norton. ISBN 978-0-393-91939-4, kurasa 194–95; picha 7.6a–c
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gneiss kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.