Grace Ogot

Grace Ogot ni mwanasiasa kutoka nchi ya Kenya.

Faili:Grace Ogot writer and mp.jpg
Grace_Ogot_writer_and_mp

WasifuEdit

Grace Ogot alipozaliwa alipewa jina la Grace Emily Akinyi katika sehemu wilayani Asembo, katika mkoa wa Nyanza. Alifanya mafunzo kama muuguzi nchini Uganda na Uingereza. Alifanya kazi kama mkunga, kama mwalimu, kama mwandishi wa habari, kama mtangazaji wa huduma ya Ng'ambo ya BBC, na katika cheo cha usimamizi katika kampuni ya Air India Corporation ya Afrika Mashariki. Mwaka wa 1984 akawa moja wa wanawake wachache kuhudumu kama Mbunge na mwanamke wa kipekee aliyehudumu kama Naibu Waziri katika Baraza la Mawaziri la Rais Daniel arap Moi. Tangu wakati huo Ogot ameshikilia nyadhifa mbalimbali za ubalozi kwani ameiwakilisha nchi yake katika Umoja wa Mataifa na UNESCO. Ogot alikuwa mwanachama mwanzilishi wa Shirika la Waandishi wa Kenya maarufu kwa Kiingereza kama Writers' Association of Kenya.

Alifunga ndoa na mwanahistoria Profesa Bethwell Allan Ogot, Mluo kutoka sehemu ya Gem, mnamo mwaka wa 1959, na ni mama wa watoto wanne.

Kitabu cha kwanza cha Grace Ogot kilikuwa Land Without Thunder , kitabu cha hadithi fupi. Riwaya yake ya kwanza ilikuwa The Promised Land . Vitabu vyake vingine ni pamoja na: The Strange Bride , The Graduate , The Other Woman na The Island of Tears .

Grace Ogot anaweza kusemekana kuwa mmoja ya waandishi bora zaidi barani Afrika. Mtindo wake wa uandishi wake ni wa kuvutia sana hasa katika ubunifu wake wa wazi ; yeye huweza kuonyesha Utabibu wa mila na tamaduni ya Kiafrika, yanayofuata njia mwafaka na ishara.

Hadithi zake nyingi zimeandikwa kutokana na historia ya Ziwa Victoria na mila na tamaduni za watu Waluo. Nathari yake ni nathari ya ubunifu ya hadithi za mila na tamaduni za kale - kama katika The Strange Bride , riwaya kuhusu mwanamke (ambaye ni mhusika mkuu) mwenye nguvu,kipawa na tabia ya kuwavutia wanaume katika nchi ya Waluo. Grace Ogot pia hukabiliana na masuala ya uhamiaji - kama ilivyo katika The Promised Land , riwaya ambayo msingi wake ni miaka ya 1930, ambapo wahusika wake wakuu wanahama kutoka Mkoa wa Nyanza hadi kaskazini mwa Tanzania, huku wakitafuta wa ardhi rutuba na mali. The Graduate pia ni riwaya kuhusu mambo magumu ya uhamiaji; katika riwaya hiyo, mhusika mkuu wa kiume anarudi kutoka Marekani hadi nchi ya Kenya, baada ya kumaliza masomo yake. Hadithi nyingi fupi katika Land Without Thunder misingi yao ni nchi ya Waluo ya kale; Maelezo ya Ogot, zana za fasihi na mtiririko wa hadithi hutoa thamani muhimu katika utamaduni na mila ya Waluo kabla ya ukoloni katika Afrika Mashariki. Ogot amechapisha kazi katika lugha za Kiingereza na Kiluo - baadhi za kazi zake zilichapishwa kwanza kwa lugha ya Dholuo.

Alihojiwa mwaka wa 1974 na Lee Nichols wa chombo cha habari cha Voice of America kwa ajili ya tangazo la redio ambalo liliwekwa hewani kati ya miaka ya 1975 na1979 (makala ya mazungumzo ya redio ya Voice of America na waandishi wa Afrika, no. . 23). Maktaba ya Bunge ina nakala ya kanda hiyo ya utangazaji na mahojiano asili ambayo hayajafanyiwa mabadilisho yoyote. Ukurasa wa utangazaji huo unaweza kupatikana katika kitabu Conversations with African Writers (Washington, DC: Voice of America, 1981), uk 207-216.

Makala ya Mwandishi huyuEdit

Kutoka mkusanyiko wa Maktaba ya Bunge, Washington, DC:

  • Aloo TLD Apul-Apul (1981) katika Kiluo.
  • Ber wat (1981) katika Kiluo.
  • The graduate (1980)
  • The Island of Tears (1980)
  • Land without Thunder,hadithi fupi (1968)
  • Miaha (1983) katika Kiluo; kilitafsiriwa kama The strange bride na Okoth Okombo (1989) ISBN 996646865X
  • The other woman : selected short stories (1976)
  • The Promised Land : riwaya (1966)
  • The strange bride kilitafsiriwa kutoka Dholuo na Okoth Okombo.