Gradi
Gradi (kutoka neno la Kifaransa) ni kizio cha kupimia pembe . Msingi wake ni mzunguko kamili wa duara unaogawiwa kwa sehemu 400ᵍ. Kwa kawaida gradi moja huandikwa kama 1ᵍ.
Nusuduara ina 200ᵍ. Pembemraba ina 100ᵍ. Jumla ya pembe ndani ya pembetatu ni 200ᵍ, ndani ya mstatili ni 400ᵍ.
Gradi inaweza kugawiwa tena kwa dakika ya tao na sekunde ya tao. Dakika ya tao 1ᶜ ni sehemu ya 100 na sekunde ya tao 1ᶜᶜ ni sehemu ya 10000 ya gradi moja.
Historia
haririAsili ya hesabu hii huaminiwa kuwa katika Ufaransa.
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gradi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |