Grand Canyon ni korongo maarufu huko Arizona nchini Marekani. Linaundwa na Mto Colorado uliochimba tangu miaka milioni kadhaa bonde lenye kina kirefu katika miamba ya nyanda za juu za Colorado.

Grand Canyon.
Mtazamo mwingine wa Grand Canyon.

Grand Canyon huwa na urefu wa km 446 na upana hadi km 29. Kuna sehemu ambako ina kina cha mita 1830 [1].

Imeandikishwa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO [2] ikiwa pia Hifadhi ya Taifa ya Marekani.

Utalii hariri

Miaka Wageni [3]
kabla ya Vita Kuu ya Pili > 100,000
1965 Milioni 1.6
2000 Milioni 4

Korongo hilo ni kati ya vivutio vikubwa kwa watalii nchini Marekani. Kila mwaka inatembelewa na wageni milioni kadhaa wanaofika kutoka ndani na nje ya nchi ya Marekani.

Marejeo hariri

  1. Kiver, E.P.; Harris, D.V. (1999). Geology of US Parklands. Wiley. uk. 902. 
  2. UNESCO, "Grand Canyon National Park"; retrieved 2012-4-18
  3. Diercke 8. Besucherentwicklung im Grand Canyon Nationalpark.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Grand Canyon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.