Eneo la Pibor

(Elekezwa kutoka Greater Pibor)

Eneo la Pibor ni eneo maalumu la kiutawala nchini Sudan Kusini. [1] Lilimegwa na Jimbo la Jonglei.

Eneo la Pibor ndani ya Sudan Kusini.

Historia

hariri

Tangu mwanzo wa uhuru wa Sudan Kusini, watu wa Anyuak, Jie, Kachepo, na Murle huko Jonglei walitafuta uhuru zaidi kutoka kwa serikali ya Jimbo la Jonglei lililotawaliwa na Wanuer na Wadinka. Uasi ulitokea kwa kutumia silaha dhidi ya Serikali ya Sudan Kusini.

Mazungumzo ya amani katika mwaka wa 2014 yalileta maafikiano ambayo yaliunganisha maeneo mawili ya Pibor na Pochalla ndani ya jimbo la Jonglei kuwa eneo jipya la kiutawala la Greater Pibor (GPAA) linalojiendesha yenyewe. [2]

Kati ya miaka 2015 hadi 2020 eneo hilo maalum la utawala lilikuwa Jimbo la Boma [3] [4] [5] lakini tangu kurudishwa kwa majimbo 10 ya kiasili limekuwa tena eneo maalum la kiutawala lililopo moja kwa moja chini ya serikali kuu.[6]

Makao makuu ya eneo hilo ni Pibor. Idadi ya wakazi wa mji wa Pibor ilikadiriwa kuwa chini ya watu 1,000 kwenye mwaka wa 2005.

Mji wa Pochalla katika wilaya ya Pochalla uko moja kwa moja kwenye mpaka wa Ethiopia. Mji uko takriban kilomita 470 kutoka Juba kupitia barabara.

Wakuu wa eneo

hariri
Kipindi Jina Chama
31 Agosti 2005 - 30 Desemba 2005 Akot Madhi SPLM
30 Desemba 2005 - 21 Mei 2011 Akot Madhi SPLM
Mei 2011 - Machi 2013 Kuol Monyluak Dak SPLM
Februari 2013 - Juni 2020 David Yau Yau SPLM
Juni 2020 - Julai 2021 Joshua Konyi
Julai 2021 - sasa Lokali Ame Bullen [7]

Marejeo

hariri
  1. "South Sudan's GPAA official refutes contest for governorship seat". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-12. Iliwekwa mnamo 2023-03-19.
  2. Todisco, Claudio (Machi 2015). LeBrun, Emile (mhr.). "Real but Fragile: The Greater Pibor Administrative Area" (PDF). Small Arms Survey (35). Graduate Institute of International and Development Studies. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2015. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Yau Yau Dissolves Part and Officially Joins SPLM", Gurtong, 12 January 2016. Retrieved on 14 August 2016. Archived from the original on 2017-04-05. 
  4. "Calm in Pibor after tension over 'disarmament' and governor", Eye Radio, 2 February 2016. Retrieved on 14 August 2016. 
  5. "South Sudan's President appoints 28 Governors, defies peace agreement", South Sudan News Agency, 24 December 2015. Retrieved on 2023-03-19. Archived from the original on 2016-09-22. 
  6. "After 6 years of war, will peace finally come to South Sudan?".
  7. "Pibor welcomes new administrator".
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eneo la Pibor kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.