Hannah Forster (mwanaharakati)

Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Gambia (195x -)

Hannah J. Forster (alizaliwa mwishoni mwa miaka ya 1950) ni mwanaharakati wa haki za binadamu wa nchini Gambia .

Maisha hariri

Forster alisoma shule ya St. Joseph's Preparatory School na St. Joseph's High School.

Baada ya kufanya kazi ya ofisi kwa muda mfupi, alifanya kazi katika maktaba ya Taifa ya Gambia . Alihitimu kutoka Chuo kikuu cha Ghana na kupata shahada ya sayansi ya maktaba na pia alihitimu kutoka Chuo kikuu cha Loughborough huko Uingereza na kupata shahada ya kwanza katika masuala ya maktaba na sayansi ya habari . Katika shule ya Sant'Anna ya mafunzo ya juu, alipata shahada ya uzamili katika masuala ya Haki za kibinadamu na kudhibiti migogoro. [1]

Marejeo hariri

  1. "Hannah Forster - African Development Bank". African Economic Conference. 2019-01-22. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 January 2019. Iliwekwa mnamo 2021-03-20.  Check date values in: |archivedate= (help)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hannah Forster (mwanaharakati) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.