Hidalgo (jimbo)
Hidalgo ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kati ya nchi. Imepakana na San Luis Potosí, Veracruz, Puebla, Tlaxcala, Mexico na Querétaro. Mji mkuu na mji mkubwa ni Pachuca.

Mahali pa Hidalgo katika Mexiko
Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 2,345,514. Una eneo la 20,502 km².
Jina la jimbo lilitolewa kwa heshima ya kiongozi wa uhuru wa Mexiko Miguel Hidalgo y Costilla.
Gavana wa jimbo ni Miguel Ángel Osorio Chong.
Lugha rasmi ni Kihispania.
Miji MikubwaEdit
- Pachuca (275,578)
- Tulancingo (96,538)
- Ixmiquilpan (73,903)
Viungo vya NjeEdit
- (Kihispania) Estado de Hidalgo Sitio oficial
Faili:Miguel Osorio Chong.JPG
Miguel Ángel Osorio Chong, gavana wa jimbo
Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hidalgo (jimbo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |