Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate

Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate iko kusini mwa Ziwa Naivasha nchini Kenya, kaskazini magharibi mwa Nairobi. Mbuga ya Taifa ya Hell's Gate inapata jina lake kutokana na vifusi vyembamba vilivyovunjika kutoka kwa miinuko, kwa wakati mmoja ilikuwa vijito vya ziwa la kale lililolisha binadamu wa kwanza katika Bonde la Ufa. Ilianzishwa mwaka wa 1984. Mbuga hii ndogo inajulikana kwa wingi wake wa aina ya wanyamapori na kwa ajili mandhari yake. Hii ni pamoja na minara ya Fischer's Tower na Central Tower na Giba ya Hell's Gate. Hifadhi hii ya Taifa pia ni makao ya vituo vitatu vya nishati za mvuke zilizoko Olkaria. Hifadhi hii ina kambi tatu msingi na inajumuisha a Kituo cha Utamaduni wa Wamasai, kinachotoa elimu kuhusu kabila la Wamasai, utamaduni na mila zake.

Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate
Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate
Hell's Gate National Park
Mahali pa Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate
MahaliMkoa wa Bonde la Ufa, Bendera ya Kenya Kenya
Nearest cityNairobi
Coordinates

0°54′57″S 36°18′48″E / 0.91583°S 36.31333°E / -0.91583; 36.31333{{#coordinates:}}: cannot have more than one primary tag per page

Eneo68.25 km²
Kuanzishwa1984[1]
Mamlaka ya utawalaKenya Wildlife Service

Historia

hariri

Hell's Gate National Park ilipata jina lake kutokana na kuvunjika kwembamba kwa miamba yake, ambayo kwa wakati mmoja ilikuwa vijito vya ziwa la kale lililolisha binadamu wa awali katika Bonde la Ufa. Ilipokea jina la "Hell's Gate" kutoka kwa Wapelelezi Fisher na Thomson mwaka wa 1883[2].

Katika miaka ya kwanza ya 1990, Mlima Longonot ulilipuka, na majivu yake bado yanaweza kupatikana ndani ya Hell's Gate.[2] Stesheni ya mvuke ya Olkaria, ya kwanza ya aina yake barani Afrika, ilianzishwa mwaka wa 1981 na nishati za mvuke huzalisha chini ya Hell's Gate kutoka maeneo ya chemchemi za majimoto. Hifadhi hii ilifunguliwa rasmi mwaka wa 1984.[3]

Jiografia

hariri
 

Mbuga ya Taifa ya Hell's Gate imekalia eneo square kilometre 68.25 (sq mi 26) ndogo kiasi kwa viwango vya Afrika.[4] Hifadhi hii iko futi 5000 juu ya usawa wa bahari.[1] Iko ndani ya Wilaya ya Nakuru, karibu na Ziwa Naivasha na wastani kilometre 90 (mi 56) kutoka Nairobi. Mbuga iko baada ya kilometre 14 (mi 9)mpinduko wa zamani katika barabara ya Nairobi kwenda Naivasha, na ina hali ya hewa ya joto na ukavu. Volkano za zamani za Olkaria na Hobley, zilizoko katika mbuga hii zinaweza kuonekana pamoja na miundo ya obsidian kutoka kwa mawe yaliyoyeyushwa na volkano kisha kupoa.[4] Ndani ya Hell's Gate kuna Giba ya Hells Gate, na kuzungukwa na miamba miekundu ambayo ina hasho mbili za volkeno: Fischer's Tower na Central Tower.[4] Kutoka kwa Central Tower kuna giba ndogo ambayo huelekea kusini na njia hushuka kutoka kwayo hadi katika chemchemi moto.[5]

Viumbe wa mwituni

hariri

Kuna aina mbalimblai za wanyamapori katika mbuga hii, ingawa nyingi zake ni chache kwa idadi.[4] Mifano ya wanyamapori wanaoonekana kidogo ni pamoja na simba, chui na duma.[6] Hata hivyo, mbuga hii kihistoria imekuwa muhimu kama makao kwa tai nadra aina ya tumbusi mlakondoo. Kuna zaidi ya aina 103 za ndege katika Hifadhi hii, zikiwa ni pamoja na tai nderi, shakivale tumbo-jeupe, na barawai.[3] Perere,[5] Mbogo, punda milia, mbungu, kongoni, swara tomi na pia nyani hupatikana kwa kawaida.[6] Hifadhi hii pia ni nyumbani kwa idadi ndogo ya korongo aina ya ngurunguru na tohe-milima.[2]

Utalii

hariri

Mbuga hii ni maarufu kutokana na ukaribu wake na Nairobi na pesa kidogo za kiingilio ikilinganishwa na mbuga nyingine za Taifa.[4] Kutembea, kuendesha baiskeli, na kuendesha pikipiki ni shughuli zinazoruhusiwa ndani ya Hifadhi,[4] jambo ambalo linaloruhusiwa katika hifadhi moja au mbili za taifa nchini Kenya.[2] Gazeti la Daily Nation lilisifia kupanda mlima katika Hell's Gate kama "wa kusisimua". Pia lilipendekeza kituo cha Joy Adamson na kuendesha boti katika Ziwa Naivasha.[7] Kituo cha Kitamaduni cha Wamasai hutoa elimu kuhusu kabila la Kimasai utamaduni na mila zao.[5]

Hifadhi hii ina kambi tatu msingi. Pia kuna pumziko kadhaa karibu na Ziwa Naivasha, maarufu miongoni mwa watalii kwa michezo ya maji, ndege na kutazama wanyama katika mashamba ya kibinafsi na kufanya matembezi katika Crescent Island, Crater Lake, na Mlima Longonot.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 World Database on Protected Areas – Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "Safari in Kenya - Hell's Gate National Park". Webkenya. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-13. Iliwekwa mnamo 2008-06-17.
  3. 3.0 3.1 "The Living Africa: National Parks - Kenya - Hell's Gate National Park". library.thinkquest.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-06. Iliwekwa mnamo 2008-06-08.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 Hodd, Michael (2002). East Africa Handbook: The Travel Guide. Footprint Travel Guides. uk. 152. ISBN 1900949652.
  5. 5.0 5.1 5.2 Hodd, 153.
  6. 6.0 6.1 Trillo, Richard (2002). The Rough Guide to Kenya. Rough Guides. ku. 243–244. ISBN 1858288592. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help); line feed character in |coauthors= at position 35 (help)
  7. Njuguna, Michael. "Kenya: Sh31m Airstrip Set to Uplift Growth of Tourism in Region", The Daily Nation, AllAfrica. Retrieved on 2009-01-24. 

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: