Hifadhi ya Taifa ya Upper Niger

Hifadhi ya Taifa ya Upper Niger ni mbuga ya taifa nchini Guinea ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali mnamo Januari 1997 kuwa kama hifadhi ya taifa ikiwa na eneo la kilomita za mraba 554 . [1]

Picha ya Hifadhi ya Taifa ya Upper Niger
Picha ya Hifadhi ya Taifa ya Upper Niger

Hifadhi hii inalinda maeneo muhimu ya misitu na savanna, na inachukuliwa kuwa ni kipaumbele cha uhifadhi katika Afrika Magharibi kwa ujumla.

Maeneo yenye athari ndogo za binadamu ni nadra sana kwa sasa nchini Guinea, na yanapatikana tu katika maeneo yenye msongamano mdogo wa watu . Eneo mojawapo ni lile la Msitu wa Mafou, eneo la mwisho lililosalia la msitu mkavu nchini Guinea na mojawapo ya machache yaliyosalia Afrika Magharibi. Eneo hili lina idadi ndogo ya watu kwa sababu ya kuenea kwa matukio ya upofu wa mto na kama matokeo ya ukatili wa Samory Touré katika sehemu ya mwisho ya karne ya 19. Eneo hilo limekuwa na usumbufu mdogo katika miaka 50 iliyopita. Hifadhi hii inajumuisha kanda mbili, eneo la ulinzi na eneo la buffer ambalo watu wa ndani wanahimizwa kutumia rasilimali za sehemu hiyo kwa njia endelevu. Kilimo na ukusanyaji wa mazao ya misitu yasiyo ya mbao yanaruhusiwa. Serikali inasimamia uvuvi, uwindaji na uvunaji wa mbao kwa ushirikiano na jamii za wenyeji. Tangu 2005, eneo lililohifadhiwa linachukuliwa kuwa Kitengo cha Uhifadhi wa Simba . [2]

Marejeo hariri

  1. Brugiere, D. and Magassouba, B. (2003). "Mammalian diversity in the National Park of Upper Niger, Republic of Guinea–an update". Oryx 37 (1): 19. doi:10.1017/s0030605303000048.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help)
  2. IUCN Cat Specialist Group (2006). Conservation Strategy for the Lion West and Central Africa. Yaounde, Cameroon: IUCN.