Historia ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Historia ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inahusu zaidi eneo la Afrika ya Kati ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Historia ya kale hariri

Ukoloni wa Ufaransa hariri

Kwa sababu ya utapakazi wa eneo kwa mabia ya mto Ubangi na mto Shari, Wafaransa wakati wa ukoloni waliita nchi hii Ubangi-Shari (Oubangui-Chari kwa Kifaransa).

Ilipokuwa koloni la Ufaransa, Ubangi-Shari ziliwekewa mamlaka ya madaraka kama eneo la Jamii ya Wafaransa mwaka wa 1958, lakini baadaye ilipata uhuru tarehe 13 Agosti 1960.

Baada ya uhuru hariri

Kwa miongo mitatu kutoka uhuru, ‘Jamhuri ya Afrika ya Kati’ ilitawaliwa na serikali za mabavu zilizonyakua mamlaka bila kufuata taratibu za demokrasia.

Kwa namna ya pekee Jean-Bédel Bokassa alitawala kuanzia tarehe 31 Desemba 1965 hadi Septemba 1979, akijifanya kaisari tarehe 4 Desemba 1976.

Mwaka wa 1993, kura za kidemokrasia za kwanza zilifanywa na kumchagua Ange-Félix Patassé kuwa Rais. Lakini Rais Patassé alipinduliwa na Jenerali François Bozizé mwaka wa 2003. Baadaye huyo alishinda uchaguzi mnamo Mei 2005 na kuiongoza nchi mpaka Machi 2013 alipolazimika kukimbia.

Kati ya Novemba 2012 na tarehe 23 Julai 2014 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipamba kwa ukatili.

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.