Historia ya Lebanoni
Historia ya Lebanoni inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Lebanoni.
Baada ya kusambaratika kwa milki ya Waturuki Waosmani kutokana na Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, Lebanoni iliwekwa na Shirikisho la Mataifa iwe chini ya usimamizi wa Ufaransa.
Nchi hiyo ilipokuwa chini ya Ujerumani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Lebanoni ilijitangazia uhuru wake mwaka 1943.
Wenyeji wana damu mchanganyiko sana, lakini lugha ya kawaida na lugha rasmi ni Kiarabu.
Kati ya nchi za Waarabu Lebanoni ni nchi pekee yenye wakazi wengi ambao ni Wakristo wa madhehebu mengiː walau ilikuwa hivyo hadi miaka ya karibuni, kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka vilivyofanya zaidi ya nusu ya Walebanoni wote wahame nchi, wakiwemo hasa Wakristo.
Kinyume chake, nchi imewapokea wakimbizi zaidi ya milioni 1, wengi wao wakiwa Waislamu.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Lebanoni kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |