Waturuki
Waturuki (kwa Kituruki: Türk, wingi: Türkler) ni jumuiya 70 hivi za watu wanaotumia lugha ya Kituruki au mojawapo ya lugha zilizo karibu. Si muhimu kwao urithi wa kinasaba (DNA), kwa maana asili zao ni tofauti sana, ila polepole waliunganishwa na lugha, utamaduni na dini.

Waturuki: Mehmed II- Suleiman Mkuu - Mustafa Kemal Atatürk - Sabiha Gökçen - Wakinadada Pekinel
Cahit Arf - Nazım Hikmet - İdil Biret - Oktay Sinanoğlu - Şebnem Ferah
Cahit Arf - Nazım Hikmet - İdil Biret - Oktay Sinanoğlu - Şebnem Ferah
Kwa maana nyingine ni jina la raia wote wa nchi ya Uturuki. Wakazi wa Uturuki ni milioni 78 hivi, lakini si wote Waturuki kiutamaduni: wengine (20-30%) ni Wakurdi, halafu Waarabu, Waarmenia n.k.
Waliohamia nje ya Uturuki pamoja na watoto wao ni takriban milioni 7: wengi wao wako Ujerumani.
Waturuki walio wengi ni Waislamu Wasunni, lakini kuna tofauti kati yao. Wengine (labda 25%) ni Waalevi ambao ni tawi la Washia.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waturuki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |