Homa ya Zika (kwa Kiingereza Zika fever) ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Zika, jamii ya jenasi Flavivirus.

Mwasho unaoendana na homa ya Zika.

Dalili zake zinafanana na zile za virusi vingine vya jenasi hiyo, kama vile Homa ya dengue au alfavirusi chikungunya, lakini ni afadhali kidogo na kwa kawaida zinadumu siku 4 hadi 7 tu. Asilimia kubwa (60–80%) hazina dalili za pekee.[1]

Wagonjwa wenye dalili wana homa kidogo, conjunctivitis, maumivu ya muda kwenye jointi (hasa zile ndogo za mikononi na miguuni) na mwasho ambao mara nyingi unaanza usoni na kuenea katika mwili wote.

Pamoja na kwamba ugonjwa huo hauna dalili za kutisha, wataalamu wa afya wanauhusisha na tatizo la microcephaly kwa mimba za wanawake wanaopatwa, kama ilivyoonyeshwa na mlipuko wa mwaka 2015 nchini Brazil ambao mwaka 2016 unazidi kuenea barani Amerika.[2][3][4][5][6][7][8][9][10][11][12]

Katika mlipuko uliotokea huko Polinesia ya Kifaransa kulikuwa na ongezeko la Guillain–Barré syndrome.[1][13]

Ugonjwa unaenezwa na mbu wa jenasi Aedes, hasa Aedes aegypti, lakini pia A. africanus, A. coargenteus, A. luteocephala,[14] A. vitattus na A. furcifer. During the 2007 outbreak on Yap Island in the South Pacific, Aedes hensilli was the vector, while Aedes polynesiensis spread the virus in French Polynesia in 2013.

Pia zimethibitishwa habari za kwamba ngono inaweza kusababisha ambukizo, na vilevile uchangiaji wa damu na uzazi (wakati wa kujifungua).[15]

Mnamo Desemba 2016, mhusika mkuu wa udhibiti wa maradhi ya namna hii nchini Tanzania aliripoti kuhusu idadi ya wakazi ambao walipimwa na kuonekana kupatwa na homa ya Zika pamoja na idadi ya watoto wachanga waliozaliwa na ulemavu kutokana na homa hiyo. Mara moja rais John Magufuli alimuengua.

Tanbihi hariri

  1. 1.0 1.1 Factsheet for health professionals. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-12-23. Iliwekwa mnamo 22 December 2015.
  2. Schnirring, Lisa. "Zika virus spreads to more countries", 30 November 2015. Retrieved on 11 December 2015. 
  3. Microcephaly in Brazil potentially linked to the Zika virus epidemic, ECDC assesses the risk, http://ecdc.europa.eu/en/press/news/_layouts/forms/News_DispForm.aspx?ID=1329&List=8db7286c-fe2d-476c-9133-18ff4cb1b568&Source=http%3A%2F%2Fecdc.europa.eu%2Fen%2FPages%2Fhome.aspx Archived 21 Januari 2016 at the Wayback Machine.
  4. "Zika virus: Health alerts in South America and Caribbean following fears illness may cause birth deformities" http://www.independent.co.uk/news/world/americas/health-alerts-in-south-america-and-caribbean-following-fears-spreading-zika-virus-may-cause-birth-a6740301.html
  5. "Brazil reports 739 suspected microcephaly cases in nine states" http://agenciabrasil.ebc.com.br/en/geral/noticia/2015-11/brazil-reports-739-suspected-microcephaly-cases-nine-states
  6. Ministério da Saúde divulga boletim epidemiológico.
  7. Oliveira Melo, A. S.; Malinger, G.; Ximenes, R.; Szejnfeld, P. O.; Alves Sampaio, S.; Bispo de Filippis, A. M. (1 January 2016). "Zika virus intrauterine infection causes fetal brain abnormality and microcephaly: tip of the iceberg?". Ultrasound in Obstetrics & Gynecology 47 (1): 6–7. ISSN 1469-0705. PMID 26731034. doi:10.1002/uog.15831. 
  8. (In Portuguese) Governo confirma relação entre zika vírus e epidemia de microcefalia http://www.bbc.com/portuguese/noticias/2015/11/151127_confirma_zika_microcefalia_mdb
  9. Brazil confirms Zika virus link to fetal brain-damage outbreak, http://www.reuters.com/article/brazil-health-zica-idUSL1N13N0NH20151128#x4sFsU0kCzW0J1Uk.97
  10. (In Portuguese) País registra 1.248 casos de microcefalia e sete mortes; maioria em PE http://noticias.uol.com.br/saude/ultimas-noticias/redacao/2015/11/30/pais-tem-1248-casos-de-microcefalia-ligacao-com-virus-zika-e-confirmada.htm
  11. Brazil warns against pregnancy due to spreading virus - CNN.com. Iliwekwa mnamo 24 December 2015.
  12. Chen, T.H.; Powers, A.M.; Lanciotti, R.S.; Marfel, M.; Holzbauer, S.; Dubray, C.; Guillaumot, L.; Griggs, A.; Bel, M.; Lambert, A.J.; Laven, J.; Kosoy, O.; Panella, A.; Biggerstaff, B.J.; Fischer, M.; Hayes, E.B. (2009). "Zika Virus Outbreak on Yap Island, Federated States of Micronesia". New England Journal of Medicine 360 (24): 2536–43. PMID 19516034. doi:10.1056/NEJMoa0805715.  Missing |last1= in Authors list (help); Missing |last3= in Authors list (help); Missing |last5= in Authors list (help); Missing |last7= in Authors list (help)
  13. http://www.eurosurveillance.org/ViewArticle.aspx?ArticleId=20720
  14. Walter Reed Biosystematics Unit, Aedes luteocephala. Retrieved 1 Feb 2016.
  15. Franchini, M.; Velati, C. (November 2015). "Blood safety and zoonotic emerging pathogens: now it's the turn of Zika virus!". Blood Transfusion. PMID 26674809. doi:10.2450/2015.0187-15. Archived from the original on 2016-02-04. Retrieved 2016-02-03. 

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homa ya Zika kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.