Polynesia ya Kifaransa
Polinesia ya Kifaransa (kwa Kifaransa: Polynésie française; kwa Kitahiti: Pōrīnetia Farāni) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa katika Pasifiki ya kusini. Eneo lake ni mafunguvisiwa mbalimbali ya Polinesia.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Tahiti Nui Mare'are'a" "Tahiti kubwa katika mvuke wa dhahabu" | |||||
Wimbo wa taifa: La Marseillaise | |||||
[[Image:|250px|Lokeshen ya Polynesia ya Kifaransa]] | |||||
Mji mkuu | Papeete | ||||
Mji mkubwa nchini | Papetee | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali | Eneo la ng'ambo la Ufaransa François Hollande Édouard Fritch | ||||
Eneo la ng'ambo la Ufaransa Sikukuu ya Mapinduzi ya Ufaransa |
14 Julai (1789) | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
4,167 km² (ya 173) 12 | ||||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - 2012 sensa - Msongamano wa watu |
(ya 177) 268,270 76/km² (ya 130) | ||||
Fedha | CFP franc (XPF )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-10) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .pf | ||||
Kodi ya simu | +689
- |
Kisiwa kinachojulikana zaidi ni Tahiti pamoja na mji mkuu wake wa Papeete ambayo ni pia mji mkuu wa eneo lote.
Jiografia
haririVisiwa, funguvisiwa na atolli za Polinesia ya Kifaransa kwa jumla vina eneo la nchi kavu la km² 4,167 jumla vilivyosambazwa katika kilomita za mraba 2,500,000 za bahari.
Visiwa vyote vimegawiwa katika tarafa tano ambazo ni vikundi vya visiwa vyenye mafunguvisiwa ndani yake; ni kama zifuatazo:
- Visiwa vya Marquesas katika kaskazini, karibu zaidi na Hawaii, penye makundi mbili ya visiwa, vya kaskazini na ya kusini
- Visiwa vya Tuamoto-Gambier ni eneo kubwa la Polynesia ya Kifaransa lenye mafunguvisiwa mawili: Tuamoto (atolli 76) na Gambier (visiwa 26)
- Visiwa vya Shirika (Visiwa vya Society) 13 vyenye asili ya kivolkeno ambavyo ni sehemu yenye wakazi wengi; vimegawiwa katika tarafa mbili za:
- tarafa ya Visiwa upande wa upepo pamoja na kisiwa kikuu cha Tahiti chenye nusu ya wakazi wote wa Polynesia ya Kifaransa
- tarafa ya Visiwa mbali na upepo
- Visiwa vya Austral (Visiwa vya Kusini) vyenye mafunguvisiwa mawili: Tubuaï na Bass.
Watu
haririWakazi ni 268,270 (sensa ya mwaka 2012), ambao kati yao 2/3 ni Wapolinesia asilia na 11,9% ni Wazungu.
Kati yao wote, 68,5% wanatumia kwa kawaida lugha ya Kifaransa, iliyo lugha rasmi pekee.
Upande wa dini, 54% ni Waprotestanti, 30% ni Wakatoliki, halafu kuna Wamormoni na Mashahidi wa Yehova.
Tazama pia
hariri
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|