Hussein Ali Mwinyi

Rais wa Zanzibar

Hussein Ali Mwinyi (amezaliwa 23 Desemba 1966) ni tabibu na mwanasiasa nchini Tanzania aliyechaguliwa kuwa rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Picha ya Mwinyi.

Baada ya kipindi cha kazi ya tiba aliingia katika siasa kwa kuchaguliwa mbunge wa Mkuranga (Mkoa wa Pwani) mwaka 2000[1] akaendelea kugombea na kuchaguliwa bungeni katika jimbo la Kwahani (Zanzibar) tangu mwaka 2005.[2] Anatokea katika chama cha CCM. Mwaka 2000 akateuliwa kuwa waziri katika serikali ya Tanzania alipokuwa naibu waziri ya afya mwaka 2000-2005, halafu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mambo ya Muungano 2006 - 2008, Waziri wa Ulinzi mwaka 2008- 2012 na tena 2014 hadi 2020. Mwaka 2012 hadi 2014 alikuwa Waziri wa Afya.

Hussein Ali Mwinyi ni mwana wa rais wa zamani Ali Hassan Mwinyi. Baada ya kusoma shule za sekondari za Azania na Tambaza, mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Tiba cha Marmara huko Istanbul, Uturuki alipohitimu masomo ya tiba mwaka 1991. Aliongeza masomo kwenye chuo cha kifalme cha tiba katika hospitali ya Hammersmith huko London, Uingereza alipopata shahada za uzamili na uzamivu (PhD) mnamo 1997.

Miaka 1993-1995 alifanya kazi ya tabibu kwenye Hospitali ya Muhimbili akaendelea kuwa tabibu na mwalimu kwenye Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kwenye miaka 1998 - 2000.

Mwaka 2020 Mwinyi aliteuliwa na CCM kuwa mgombea wake kwa urais wa Zanzibar akatangazwa mshindi na kuapishwa.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Member of Parliament CV, Hussein Ali Mwinyi, tovuti la bunge la Tanzania mwaka 2015, iliangaliwa kipitia archive. org mnamo Novemba 2020
  2. "Mengi kuhusu Hussein Ali Mwinyi". 1 Februari 2007. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-19. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2011.