Igowole ni kata ya Wilaya ya Mufindi katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51409.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 18,925 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,459 waishio humo.[2]

Kuna maendeleo ya kasi sana na mji mdogo wa Igowole kwa sasa unatarajiwa kuwa makao makuu ya Wilaya ya Mufindi zitakapogawanywa na Mafinga.

Ni mji wenye vivutio: makampuni makubwa kama Unilever Tea Tanzania, viwanda kadhaa vya chai na mbao, mabwawa makubwa sana ya Ngwazi, Nzivi na Kihanga. Mashamba makubwa ya chai yapo nje kidogo ya mji.

Msitu wa Saohill upo mwanzo wa mji, hivyo mji upo kiutalii sana. Shughuli kuu za watu wa Igowole ni KAZI ZA viwandani, biashara, kilimo, shughuli za mbao, na uvuvi katika mabwawa yaliyoyatajwa na pia ndiko viliko vyanzo vya mto Ruaha.

Mitaa ya mji mdogo wa Igowole ni Ligu, Ihanga, Mhamati, Kafufu, Nyuma ya Msitu, Mahaga, Mhemi, Nzivi, na Kisasa.

Marejeo

  Kata za Wilaya ya Mufindi - Tanzania  

Idete | Idunda | Ifwagi | Igombavanu | Igowole | Ihalimba | Ihanu | Ihowanza | Ikongosi | Ikweha | Itandula | Kasanga | Kibengu | Kiyowela | Luhunga | Maduma | Makungu | Malangali | Mapanda | Mbalamaziwa | Mdabulo | Mninga | Mpanga Tazara | Mtambula | Mtwango | Nyololo | Sadani


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Igowole kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.