Wilaya ya Mufindi

Mufindi ni wilaya iliyopo katika Mkoa wa Iringa nchini Tanzania yenye Postikodi namba 51400[1]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 265,829 [2].

Mahali pa Mufindi (kijani) katika mkoa wa Iringa. Upande wa kusini umetengwa na kufanywa mkoa mpya wa Njombe.

Wilaya imepakana upande wa kaskazini na wilaya za Kilolo na Iringa Mjini, upande wa kusini na mkoa wa Njombe, upande wa mashariki na mkoa wa Morogoro na upande wa magharibi na Mkoa wa Singida.

Mufindi iko sehemu ya Nyanda za Juu za Kusini na sehemu za wilaya ziko mita 2000 juu ya usawa wa bahari. Kwa hiyo kuna baridi na mvua nyingi. Wilayani kuna mashamba makubwa ya chai, misitu ya kupandwa ya Sao Hill inayoongoza kwa kutoa mbao Tanzania na Afrika Mashariki, inastawisha mahindi, maharagwe, viazi, kabichi na pareto.

MarejeoEdit

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mufindi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Kata za Wilaya ya Mufindi - Tanzania  

Bumilayinga | Idunda | Ifwagi | Igombavanu | Igowole | Ihalimba | Ihanu | Ihowanza | Ikweha | Isalavanu | Itandula | Kasanga | Kibengu | Kiyowela | Luhunga | Makungu | Malangali | Mapanda | Mbalamaziwa | Mdabulo | Mninga (Mufindi) | Mpanga Tazara | Mtambula | Mtwango | Nyololo | Rungemba | Sadani

Tovuti za NjeEdit

  • www.facebook.com/mufindiradio
  • www.mufindiradio.com