Ilorienito ni kata ya Wilaya ya Longido katika Mkoa wa Arusha, Tanzania, yenye postikodi namba 23515. Sehemu kubwa ya kata ipo juu ya Mlima Kitumbeine hivyo hali ya hewa hufaa sana kwa kilimo na ufugaji. Kata ina misitu karibu na kilele cha mlima huo.

Vijiji vipo 3, ambavyo ni Losirwa, Iloirienito na Nadaare.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,932 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,571 [2] walioishi humo.

Wakazi wa kata ya Iloirienito hujishughulisha na ufugaji na kilimo mlimani. Wanyama wafugwao ni pamoja na ng'ombe, mbuzi, kondoo na punda.

Mazao yanayolimwa ni: maharagwe, mahindi, viazi, maboga na mboga za majani.

Kuna shule 4 za msingi na zahanati 3.

Huduma ya usafiri ni hafifu na wakazi wengi hutembea zaidi kwa miguu.

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Arusha - Longido DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-19.
  Kata za Wilaya ya Longido - Mkoa wa Arusha - Tanzania
 

Elang'atadapash | Engarenaibor | Engikaret | Gelai Lumbwa | Gelai Meirugoi | Ilorienito | Kamwanga | Ketumbeine | Kimokouwa | Longido | Matale A | Mundarara | Namanga | Noondoto | Olmolog | Orbomba | Sinya | Tingatinga


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ilorienito kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.