Injinitreni (pia: kichwa cha treni; kwa Kiingereza locomotive) ni sehemu ya treni yenye injini na nguvu ya kuvuta au kusukuma treni yote. Ni kama gari kubwa lisilobeba abiria wala mizigo. Badala yake inabeba ndani yake injini moja au zaidi kubwa pamoja na tangi.

"Gari la mooshi - injinitreni ya mvuke

Aina za injinitreni

Injinitreni diseli

 
Katika mazingira ya milima injiniterni 3 zimeunganishwa pamoja kuvuta treni ndefu haraka

Injinitreni ya diseli huwa na injini ya diseli. Kuna aina mbili

Injinitreni ya mvuke

 
Injinitreni ya mvuke

Injinitreni ya mvuke hutumia joto la kuwasha kuni, makaa au mafuta kuchemsha maji na kusukuma injini kwa nguvu ya mvuke wa maji.

Hii ilikuwa aina asilia ya injinitreni lakini siku hizi hazitumiwi tena, isipokuwa mahali pachache kwa ajili ya maonyesho au utalii.

Injinitreni ya umeme

 
Injinitreni umeme ya A GG1

Katika nchi nyingi injinitreni zinatembea kwa nguvu ya umeme inayopatikana kwa njia ya nyaya za umeme kando ya njia ya reli.

Aina hii ina gharama ndogo kwa harakati lakini gharama ni kubwa kujenga nyavu za umeme kando ya njia za reli.