Irenei wa Srijem (alifariki Sirmium, leo Srijem nchini Korasya[1], 6 Aprili 304) alikuwa askofu kijana aliyepigwa mijeledi, akateswa gerezani siku nyingi na hatimaye akakatwa kichwa kwa sababu ya imani yake katika dhuluma ya kaisari Maximian.

Hakujali mateso hayo yaliyotangulia wala mabembelezo ya wazazi, mke na watoto wake[2].

Ndiyo maana anaheshimiwa tangu zamani na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 6 Aprili[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. The Oxford Handbook of Late Antiquity edited by Scott Fitzgerald Johnson, p.98-99
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/48580
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Walsh, Michael, ed. Butler's Lives of the Saints.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.