James Gayo
James Gayo ni msanii kutoka nchini Tanzania anayejulikana sana kwa uchoraji wa katuni ya Kingo. Amejipatia umaarufu kwa katuni hii ya Kingo kufuatiliwa katika nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda na Zambia. [1]
Elimu
haririGayo alisoma huko jijini Mwanza na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi.
Alipata nafasi ya kuendelea kielimu na kujiunga na shule ya sekondari hukohuko jijini Mwanza. Katika elimu yake ya sekondari alikutana na mtaalamu katika uchoraji RJ Kapera aliyeweza kumsaidia kukuza kipaji chake baada ya kuacha shule.
Alifanya kazi pamoja na Kapera kwa takribani miaka mitatu. Baadaye Gayo aliweza kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi mnamo mwaka 1980 mpaka mwaka 1982 ambapo alitunukiwa diploma katika ubunifu na uchoraji.
Gayo hakuishia hapo, aliweza kujiunga na Chuo cha Ushauri wa Sanaa kilichopo katika jiji la Dar es Salaam kwa miaka mitatu na kuacha baada ya kupata ufadhili wa masomo wa kwenda nchini Uswisi na kuwa mmoja kati ya Watanzania wawili waliofanikiwa kuhitimu kujifunza nchini Uswidi. [2]
Kazi
haririPindi aliporudi nchini Tanzania kutokea Uswidi, Gayo aliweza kufanya kazi na mojawapo ya kampuni zilizopo jijini Dar es Salaam huku akiwa anafanya kazi kama mfafanusi wa michoro.
Mwishoni mwa mwaka 1990, Gayo aliamua kutilia msisitizo katika uchoraji wa katuni zake ambazo aliamini kwamba zitamfikisha mbali.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.lambiek.net/artists/g/gayo_james.htm
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-08. Iliwekwa mnamo 2019-04-08.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu James Gayo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |