Mwanza (mji)

Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 378,327 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).

Picha ya angani ya Mji wa Mwanza
Jiji la Mwanza
Jiji la Mwanza is located in Tanzania
Jiji la Mwanza
Jiji la Mwanza
Mahali pa mji wa Mwanza katika Tanzania
Majiranukta: 2°31′5″S 32°53′53″E / 2.51806°S 32.89806°E / -2.51806; 32.89806
Nchi Tanzania
Mkoa Mwanza
Wilaya Ilemela
Nyamagana
Idadi ya wakazi
 - 378 827
Wilaya za Jiji la Mwanza

Jiji hili limekuwa na vivutio mbalimbali vikiwemo mawe yaliyo katika Ziwa Victoria katika eneo la Nyanza. Pia jirani kuna hifadhi za wanyama wa porini kama Sanane, ambapo kuna wanyama kama simba, swala, pundamilia, sokwe,duma na chui

HistoriaEdit

Mwanza ilianzishwa na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mahali paliteuliwa kutokana na nafasi ya bandari asilia upande wa kusini ya Ziwa Viktoria. Wajerumani waliuita mji kwa jina "Muansa" inaaminiwa ilikuwa matamshi yao ya neno "nyanza". Walijenga boma kubwa iliyoendelea kitovu cha mji. Takwimu ya Kijerumani ya 1912 ilihesabu wazungu 85, Wagoa 15, Wahindi wengine 300 na Waarabu 70 lakini haikutaja wakazi Waafrika. Palikuwa na makampuni ya biashara 12 ya kizungu na 50 ya Wahindi.[1].

MarejeoEdit

  1. Koloniallexikon makala "Muansa"
  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mwanza (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
  Kata za Jiji la Mwanza - Mkoa wa Mwanza - Tanzania  

Wilaya ya Ilemela: BugogwaBuhongwaBusweluButimba (Ilemela)IgomaIlemelaMkolaniNyakatoPasiansiSangabuye
Wilaya ya Nyamagana: IgogoIsamiloKirumbaKitangiriMbuganiMirongoMkuyuniNyamaganaNyamanoroPamba